Heri niolewe na mwizi-Huddah Monroe afichua kwa nini atapendelea kuolewa na jambazi

Muhtasari
  • Huddah amekuwa akivuma kwa muda sasa mitandaoni, kwa kuwakosoa wanaume vikali kwa kutojua kupenda
Screenshot.from.2019.10.17.12.37.26
Screenshot.from.2019.10.17.12.37.26

Mmoja wa mwanamke mashuhuri na mjasiriamali wa Kenya Huddah Monroe amezua tafrani tena mtandaoni baada ya kufichua hadharani kwamba anapendelea sana kuolewa na jambazi ikilinganishwa na mtu wa kanisani.

Kwa mujibu wa Huddah Monroe wengi wa watu hususani watu mashuhuri kama vile wanasiasa na pia wachungaji ambao ni watu wa Mungu wana historia ya kuhusika katika kashfa ambazo zinaweza kuitwa wizi ama kwa unyakuzi, ufisadi au matumizi mabaya ya fedha za umma.

Huddah amekuwa akivuma kwa muda sasa mitandaoni, kwa kuwakosoa wanaume vikali kwa kutojua kupenda.

Pia wiki iliyopita alivuma baada ya kudaiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii kutoka Tananzania Jux.

Akiwa kwenye mahojiano mwanasosholaiti huyo alisema kwamba atafunga ndoa hivi karibuni, na kwamba wamekuwa marafiki na msanii huyo kwa muda.

"Hata wahubirii ni wezi,wanasiasa wenu ni wezi pia napendelea kuolewa na mwizi haraka sana kuliko mwanamume wa kanisani," Huddah aliandika.