"Peter alijificha katika kivuli cha Uinjilisti ili kumuua binti yangu" -Mama wa Osinachi asema

Muhtasari

•Mume wa Osinachi, Peter Nwachukwu anakabiliwa na mashtaka 23 kuhusiana na mauaji ya bila kukusudia yaliyosababisha kifo cha mwimbaji huyo.

•Mama Osinachi alitoa ushahidi mbele ya mahakama akisema Peter hakumruhusu kumtembelea binti yake kwa sababu anamwita mchawi.

Image: BBC

Mama wa aliyekuwa mwimbaji wa injili nchini Nigeria Osinachi Nwachukwu ameiambia mahakama kile kilitokea kwa binti yake wakati wa maisha yake ya ndoa na Peter Nwachukwu kabla hajafa.

Mume wa marehemu Osinachi  'alimnyanyasa binti yake na kusababisha kifo chake', Caroline Madu aliiambia Mahakama Kuu ya Abuja Jumatatu.

Kifo cha Osinachi Nwachukwu kilichotokea Aprili 2022 kilizua ghadhabu kote nchini Nigeria baada ya familia yake kudai kuwa alikabiliwa na ukatili wa majumbani kupitia mikono ya mume wake

Mume wa Osinachi, Peter Nwachukwu anakabiliwa na mashtaka 23 kuhusiana na mauaji ya bila kukusudia yaliyosababisha kifo cha mwimbaji huyo.

Madam Madu ndiye shahidi mkuu katika kesi ya Nwachukwu, mume wa marehemu mwimbaji.

Mama wa Osinachi aliangua kilio wakati akisimulia jinsi "Peter alivyoenda nyumbani kwake akijificha kama mwinjilisti".

Ni "kumuiba na kumuua binti yangu" anaiambia mahakama.

Madam Madu anasema tangu alipoolewa kwa miaka 14,alirudi nyumbani pale akiwa mgonjwa tu.

Na baada ya watu kumsihi Peter na wiki mbili baadaye, alimfukuza, aliongeza.

Mama huyo alitoa ushahidi mbele ya mahakama akisema Peter hakumruhusu kumtembelea binti yake kwa sababu anamwita mchawi.

Pia hakumruhusu mwimbaji marehemu Osinachi kuhusiana na ndugu yake yeyote, anadai.

Mama huyo alisema kwamba ugonjwa pekee ambao binti yake alikuwa nao ulikuwa ni vidonda vya tumbo.

Mama huyo ameongeza kwa kusema yeye alienda sokoni kununua bidhaa na kumpa mdogo wake Osinachi kwenda kumpadada yake baada ya kumwambia kuwa alikuwa na njaa.

Akiwa nyumbani, mume wa Osinachi alianza kumnyanyasa mvulana huyo, anaiambia mahakama.

Dada wa Osinachi pia atatoa ushahidi mbele ya mahakama Jumatatu ya Juni 20, 2022.

Alielezea korti kwamba Peter alimchukulia Osinachi kama mnyama na kumpiga.

Baada ya kuhojiwa,  wakili wa utetezi, aliiomba mahakama kuahirisha kesi.

Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa leo Juni 21

Kifo cha Osinachi Nwachukwu cha Aprili 2022 kilizua ghadhabu kote nchini Nigeria baada ya familia yake kudai kuwa anateswa nyumbani kwa mkono wa mumewe.

Kilio hicho kiliwafanya polisi wamuweke kiuzuizini mumewe kwa mahojiano kabla ya kumpeleka mahakamani.

Kwa hiyo, matokeo ya kesi ya mume wa Osinachi ni mambo ambayo watu wengi wanapaswa kuzingatia.

Wakati huohuo familia yake ya mwimbaji wa Nigeria inapanga kumzikamwimbaji huyo mwezi Juni, kulingana na ripoti.

Je, ni mashtaka gani dhidi ya mume wa Osinachi?

  •  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Shirikisho na Waziri wa Sheria ya faili ya madai ya kudai kwamba Peter alimfukuza Osinachi kwa nguvu kutoka kwa nyumba yake ya ndoa na kitendo hicho ni kinyume cha Sheria ya Unyanyasaji dhidi ya Watu, Sheria ya VAP (Marufuku), ya 2015.
  • Na kumsukuma huko kwa nguvu mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka kwenye gari linalotembea.
  • Anashtakiwa kwa kufanya mauaji bila kukusudia chini ya kifungu cha 104 na 379 cha Sheria ya Utawala wa Haki ya Jinai, 2015. Makosa hayo ni kinyume na kifungu cha 221 cha Kanuni ya Adhabu na adhabu yake ni kifo.
  •   Mshtakiwa alimnyima Osinachi uhuru wake wa binafsi huku akimzuia kutembea na kumfungia nyumbani. Sheria, 2015.
  • Mshitakiwa amemnyima Osinachi kupata pesa zake ili aende hospitali na kuzitumia katika mahitaji ya nyumbani huku akimlazimisha kuomba na kukopa. Mume wa Osinachi alimtenga kwa nguvu na na familia yake kwa kumzuia mama yake na ndugu zake kutembelea nyumbani kwao. Nwachukwu anadaiwa kumpiga mwimbaji huyo na kurekodi sauti ya kulia.
  • Ili kuzuia watu wasiache kuripoti vitendo vya unyanyasaji wa nyumbani dhidi ya wanawake." Katika kesi mahakamani leo, ninaamuru usikilizaji uharakishwe" Jaji Nwosu-Iheme atoa taarifa.
  • Mke wa Nwachukwu alifariki Aprili 8, 2022 na ndugu zake wengi walimshtumu mume wake kwa kusababisha kifo chake.
  • Polisi wa Nigeria walimkamata Nwachukwu na bado yuko kizuizini kabla hata ya kufunguliwa mashtaka.