Mume wangu! Zari Hassan katika ndoa ya tatu?

Muhtasari

•Zari Hassan anadaiwa kupendelea kujitosa kwenye  mahusiano na wanaume wenye umri mdogo kumliko.

•Mwanasoshalaiti huyo alibainisha kuwa huwa anamheshimu na hajihusishi katika shughuli zake za kazi.

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Wikendi mwanasoshalaiti Zari Hassan alitamatisha ziara yake ya ya kikazi ya siku tano nchini Tanzania.

Mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz alitua Tanzania mapema wiki jana akiwa ameandamana na mwanaume mwenye umri wa ujana.

Akizungumza na waandishi wa habari, Zari alimtambulisha mwanaume huyo, sio tu kama mpenzi wake, bali kama mume wake.

“Huyu ni mume wangu, ni mume wangu, kesi kwisha!” Zari alisema

Zari alipoulizwa sababu ya mume huyo wake kujitenga mbali naye alibainisha kuwa huwa anamheshimu na hajihusishi kamwe katika shughuli zake za kazi.

“ Niko kwenye kazi na mume wangu wangu na haingilii vitu vyangu za kazi , ananiheshimu.” Alisema

Mzaliwa huyo wa Uganda hata hivyo alikataa kufichua jina la mpenzi  wake wakati alipoombwa kufanya vile.

Hatua ya mwanasoshalaiti huyo kumtambulisha mpenzi mpyawa inajiri baada ya kuachana na mfanyibiashara wa Uganda, GK Choppa.

Wanamitandao waligundua kuwa amevunja mahusiano yake na Choppa pale alipofuta picha zao kutoka kwa ukurasa wake wa Instagram.

Mahusiano ya Zari na mfanyibiashara huyo yalizua utata mitandaoni kwani alionekana kuwa mwenye umri mdogo kumliko.

Mama huyo wa watoto watano anadaiwa kupendelea kujitosa kwenye   mahusiano na wanaume wenye umri mdogo kumliko.

Zari ni mke wa zamani wa staa wa Bongo Diamond Platinumz na walijaliwa kupata watoto wawili pamoja.

Alikiri ya kwamba iwapo Diamond Platinumz hayuko karibu kila wakati, anasaidia na kuchangia pakubwa katika malezi ya Watoto wao.

Zari pia aliwahi kuwa kwenye ndoa na mfanyibiashara wa Afrika Kusini Ivan Semwanga ambaye alifariki mwaka wa 2017.