'Mario sio mpenzi wangu,'Michelle Ntalami afunguka kuhusu uhusiano wake wa kimappenzi

Muhtasari
  • Wawili hao walionekana kupendeza huku mashabiki wakidai kwamba,Mario ndiye chumba wake wa sasa
Michelle Ntallami
Michelle Ntallami
Image: instagram/michelle

Michelle Ntalami siku ya Alhamisi aliwaacha mashabiki wwake midomo wazi huku wengi wakimpongezza baada ya kupakia picha na video akiwa na na mpenzi mpya.

Wawili hao walionekana kupendeza huku mashabiki wakidai kwamba,Mario ndiye chumba wake wa sasa.

Mashabiki na wanamitandao walidhani MItchelle amempata mpenzi mpya, hii ni baada ya miezi kadhaa baada ya kuachana na Makena Njeri.

Baada ya kuachana kwao Mitchelle hajawahi mtambulisha mpenzi mpya mitandaoni,lakini kuonekana kwa video na picha zake mitandaoni kuliwafanya wengi kudhani kwamba ana mchumba mpya.

Chipmunk akiwa ameshika mkono wa Michelle alimbusu alipogeuza kamera kwake.

"Ninahisi kupendwa tena," yalisomeka nukuu ya Michelle.

Kwenye Insta ya Chipmunk, aliandika;

"Heri ya kuzaliwa mtoto #thirtyATE Kwa kupenda, furaha, uponyaji na mwaka wako mpya @michelle.ntarami."

Michelle pia alishiriki picha nzuri kwenye ukurasa wake akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na marafiki zake wa karibu na familia.

Alitarajia kuwa na furaha katika mwaka wake mpya.

Naam, Michelle amekana kuchumbiana na Mario.

"DM yangu inavuma kwa jumbe za 'Nina furaha sana kwa ajili yako'.. Hapana, sichumbiwi na Mario. Nilisukumwa na hisia na kuhisi tu. wa kipekee wakati huo Nyie mna haraka sana, hivi ndio mnafikia hitimisho,"Michelle aliandika