"Tafadhali niongezee watoto zaidi," Brown Mauzo amsihi mkewe Vera Sidika

Muhtasari

•Mauzo amemshukuru Mungu kwa ajili ya mwanasoshalaiti huyo na kusema kuwa amebarikiwa sana kuwa na mke wake.

•Vera amewahi  kufichua anapanga kupata angalau watoto wengine watatu.

Image: INSTAGRAM// BROWN MAUZO

Mwanamuziki Brown Mauzo amemsherehekea mke wake na ambaye ni mama ya binti yake Vera Sidika.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram,  Mauzo amemshukuru Mungu kwa ajili ya mwanasoshalaiti huyo na kusema kuwa amebarikiwa sana kuwa na mke wake.

"Nimebarikiwa, Asante Mungu," Mauzo aliandika chini ya picha ya kipenzi hicho cha moyo wake.

Msanii huyo kutoka Pwani pia alitumia fursa hiyo kumuomba mkewe amzalie watoto zaidi.

"Mke mpendwa, Vera Sidika, tafadhali niongezee watoto zaidi," Aliandika.

Wawili hao wamekuwa kwenye mahusiano kwa takriban miaka miwili na tayari wamebarikiwa na mtoto mmoja pamoja. 

Binti wao, Asia Brown alizaliwa Oktoba 20, 2021. Akitangaza kuzaliwa kwa bintiye, Vera alisema kwamba Asia ataishi kuwa miujuza ambayo itakamilisha maisha yake na mumewe.

"Tarehe 20.10.2021 mida ya saa nne na dakika 21 asubuhi, mtoto wa malkia alizaliwa. Asia Brown @princess_asiabrown. Utaishi kuwa miujiza ambayo itafanya maisha yetu yawe kamili" Vera alitangaza takriban miezi minane iliyopita.

Hapo awali mwanasoshalaiti huyo amewahi kudokeza kuwa anapanga kupata mtoto mwingine hivi karibuni.

Miezi michache iliyopita Vera alifichua kwamba yeye na mumewe wanatamani sana kupata mtoto wa pili.

"Nina tamaa kubwa ya mtoto. Kweli, sio mimi tu, mume wangi  pia. Tunataka mtoto mwingine. Kwa matumaini, mvulana. Labda tunapaswa kuzingatia hilo  na kujaribu. Kwa kiwango hiki, Mtu huenda akawa mjamzito tena mwaka huu," Vera alisema..

Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 32 pia amewahi  kufichua anapanga kupata angalau watoto wengine watatu.

Vera alisema angependa kupata watoto wawili wa kiume na mwingine mmoja wa kike ili kuwe na usawa katika familia yake.

"Kusema kweli nataka watoto wanne. Natumai kupata wavulana wawili na wasichana wawili. Hivyo Asia atakuwa na dada na kaka wawili. Mvulana ambaye nitapata atakuwa na kaka na dada wawili. Huo ni usawa mzuri. Kwetu tulikuwa watatu na nilikuwa msichana pekee. Iliniuma sana kukua bila dada." Alisema.

Vera amekuwa akionyesha wazi nia yake kubwa ya kukuza familia yake na Mauzo.