"Mpenzi wangu hutazama ponografia kila siku lakini anataka tu tendo mara moja kwa mwezi" mwanadada ateta

Alisema alijaribu kuongea na mumewe kuhusu hilo tatizo lakini haijafua dafu.

Muhtasari

• "Hivi majuzi, niligundua kwamba anatazama ponografia kila siku na kupiga punyeto, ambayo hataki nijue,” mwanadada alieleza

Wanandoa kitandani
Wanandoa kitandani
Image: The Star

Kumeibuka na uvumi kwamba video za ngono hutafutwa sana mitandaoni haswa na watu wengi kutoka Mashariki ya Kati.

Haya yanajiri huku mwanamke mmoja akilalamika kwamba mumewe huwa na mazoea ya kutazama video za ngono kila wakati na jambo hilo ameshindwa vile atamshawishi kuacha.

Kuongezea chumvi juu ya kidonda kibichi, mwanamke huyo pia anaeleza kwamba hata baada ya kutazama video hizo kila muda, mumewe huwa anamuomba ngono mara moja tu kwa mwezi.

Akitafuta ushauri nasaha kwa mwanasaikolojia mmoja maarufu nchini Marekani, mwanamke huyo ambaye jina lake lilibanwa alieleza kwamba ana miaka 29 na mumewe ana miaka 32 na kwamba wamekaa katika ndoa kwa mwaka mmoja ambapo sasa hulka ya mumewe kutazama video za ngono ni kama inaelekea kuivuruga ndoa yake.

“Lakini baada ya miezi sita ilikuwa tunashiriki penzi mara moja tu kwa wiki na sasa ni mara moja tu kwa mwezi. Nilijaribu kuongea naye kuhusu ukosefu wake wa hamu lakini alisema hilo lilizidisha hali hiyo. Hivi majuzi, niligundua kwamba anatazama ponografia kila siku na kupiga punyeto, ambayo hataki nijue,” mwanamke huyo alilalama.

Mwanamke huyo alisema kweli bwanake anampenda lakini kwa upande wat endo la ndoa anamtelekeza sana na kumnyima haki yake.

Mwanasaikolojia alishauri kwamba ni vyema mwanadada huyo amegundua mapema na suala kama hili la wanaume kuchukuliwa kimawazo na video za ngono ni sugu sana ambalo muda mwingine linahitaji msaada wa mtaalamu wa masuala ya ngono na uzazi.

Ila pia alisema huenda kuna sababu maalum inayomfanya mwanaume huyo kujitenga mbali na ngono kutoka kwa mkewe na ni vizuri kufuatilia kwa utaratibu ili kubaini.

“Baadhi ya wanaume wamelazimishwa kujihusisha na ponografia kwa kiwango ambacho wanahitaji msaada wa kitaalamu. Unapaswa kuzungumza juu ya mahitaji yako na kujua kwa nini hasa mumeo amejipusha na ngono. Kunaweza kuwa na sababu ya matibabu au ya kisaikolojia, kwa hiyo jaribu kumkaribia kama msaidizi, bila lawama - na bila kudhani kwamba hajavutiwa tena na wewe,” alishauri mwanasaikolojia.

Tatizo la wanaume kuwa na mazoea ya kujiridhisha kwa kutazama video za ngono na wengine kutumia mafuta ya kujipaka kupiga punyeto limekuwa likizungumziwa sana haswa nhini Kenya, huku wanawake walioko katika ndoa wakilalamika pakubwa.