"Niko tayari kupokea yote!" Lilian Ng'ang'a adokeza mimba, apakia picha

Katika picha ambayo alikata maeneo ya tumbo kwenda chini, wapelelezi wa mitandaoni wanasema picha hiyo inaonesha ujauzito.

Muhtasari

• Lilian Ng'ang'a amekuwa kwenye mahusiano ya Juliani kwa zaidi ya miezi 6.

• Wawili hao wanasemekana kufanya harusi ya faragha miezi michache iliyopita.

Aliyekuwa mke wqa gavana Mutua
Lilian Ng'ang'a Aliyekuwa mke wqa gavana Mutua
Image: Instagram

Baada ya sema sema za wambea kwenye mitandao ya kijamii, sasa ni wazi kwamba aliyekuwa mke wa gavana wa Machakos Alfred Mutua, Lilian Ng’ang’a ni mjamizto na pamoja na mpenzi wake mpya mwanamuziki Juliani, wanatarajia kijajo.

Hili limedhibitishwa na Lilian baada ya kupakia picha yake akionekana kuwa na ujauzito, japo picha yenyewe aliikatia maeneo ya tumbo lakini muonekano kabisa unaonesha kitumbo mbele na kuifuatisha kwa ujumbe unaoashiria kwamba anatarajia mtoto hivi karibuni.

“Najua utakuwa vizuri. Niko tayari kupokea yote,” Ng’ang’a aliandika ujumbe huo wa kimafumbo kwenye picha hiyo.

Watu mbalimbali walifurika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwenye picha hiyo na kumwaya hongera zao kwa mwanamama huyo ambaye miezi michache iliyopita ilisemekana walifunga harusi ya faragha na mpenzi wake, mwanamuziki wa kuchana mistari, Juliani.

“Huu mwaka watu maarufu naona mmekataa kulala darasani. Hongereni jamani,” aliandika mmoja kwa jina Leah Apitsa.

Ng’ang’a ambaye pia anajiongeza kama mjasiriamali waliachana na gavana Mutua mwishoni mwa mwezi jana baada ya takribani miaka kumi katika mahusiano yao ambapo hawakufanikiwa kupata mtoto pamoja na siku chache baadae akaanza kuonekana akitoka kimapenzi na mwanamuziki Juliani.

Jambo hilo halikukaa sawa na gavana Mutua aliyeonekana kuumwa sana na mpaka inasemekana kwa wakati mmoja alijaribu kumtishia Juliani, suala lililoibua mjadala mkali mitandaoni huku mwanaharakati Boniface Mwangi akijitosa ndani kwa kutetea Juliani na Lilian na hivyo kuibua uhasama mkali baina yake na gavana Mutua.

Miezi michache iliyopita, Ng’ang’a aliachia kitabu alichokiandika yeye ambacho kilikuwa kinazungumzia maisha yake ya miaka karibia kumi kama mama kaunti ya Machakos na mke wa gavana.