Siamini kama Kajala ni wangu-Harmonize

Kabla ya kumvisha pete Harmonize alivuma mitandaoni kwa kumuomba Kajala msamaha hadharani

Muhtasari
  • Siku chache baaada ya kumvisha mpenzi wa maisha yake pete msanii wa bongo Harmonize akiwa kwenye mahojiano amesema kwamba bado hajaamini kwamba Kajala ni wake
Harmonize na Kajala
Harmonize na Kajala
Image: HISANI

Siku chache baaada ya kumvisha mpenzi wa maisha yake pete msanii wa bongo Harmonize akiwa kwenye mahojiano amesema kwamba bado hajaamini kwamba Kajala ni wake.

Kabla ya kumvisha pete Harmonize alivuma mitandaoni kwa kumuomba Kajala msamaha hadharani na hata kumnunulia zawadi za bei ghali ili aweze kumsamehe.

"Kuna wakati mtu huamini kabisa kinachotokea kwenye maisha yako, mimi siamini kabisa kama K (Kajala) ni wangu sasa,"Alizungumza Harmonize.

Msanii huyo alimshukuru Mungu kwa kumpa nafasi nyingine ya kuwa na mpenzi wake, huku akiai kwama kuwa au kuoa mtu ambaye anakupa raha ni zawadi ya kipekee duniani.

“Mwenyezi Mungu ni mwema sana, amenisogeza karibu kabisa na mwanamke wa maisha yangu, maana nitampenda siku zote, nampenda mno furaha ya maisha yangu ipo mikononi mwake sasa."