Briana azuru Tanzania baada ya ex wake Harmonize kumvisha Kajala pete ya uchumba

Briana alichapisha picha akiwa amesimama ufukweni mwa jiji la Dares salaam.

Muhtasari

•Briana alichapisha picha inayomuonyesha akiwa amesimama ufukweni mwa jiji la Dares salaam kuthibitisha uwepo wake.

•Ziara yake ya sasa inajiri siku chache tu baada ya Harmonize kumvisha Kajala Masanja pete ya uchumba.

Harmonize na Briana
Harmonize na Briana
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Mpenzi wa zamani wa Harmonize, Briana Jai kwa sasa yupo kwenye ziara nchini Tanzania.

Kipusa huyo kutoka Australia  aliwasili katika nchi hiyo jirani siku chache zilizopita na kuwatangazia mashabiki wake kupitia Instagram.

Briana alichapisha picha inayomuonyesha akiwa amesimama ufukweni mwa jiji la Dares salaam kuthibitisha uwepo wake.

"Je mlinimiss😜🇹🇿?" Briana aliandika chini ya picha hiyo ambayo alichapisha kwenye Instastori zake.

Hii hata hivyo sio mara ya kwanza ya kipusa huyo kuzuru Tanzania baada ya kutengana na bosi wa Konde Music Worldwide. Awali aliwahi kufanya ziara pale.

Takriban miezi minne iliyopita Harmonize alithibitisha kutengana kwake na mwanamitindo huyo aliyechumbiana naye kwa kipindi kifupi. 

Konde Boy alitaja sababu kadhaa za kuvunja mahusiano yao ikiwemo sababu kuwa bado alimpenda Kajala.

"Kuhusu Briana sina Tatizo naye kabisa, yeye ni mtu mzuri ila hatuko pamoja, sababu moja  nilimwambia nimetengana na mtu bila kugomabana na nampenda sana sasa sina uhakika kama nimemove on lolote linaweza kutokea maana itakuwa ni kitendo kizalendo pia mimi kurudi nyumbani," Alisema kupitia Instagram.

Briana alithibisha kurejea kwake nyumbani kwao Australia na kumtakia mema staa huyo wa Bongo.

Vilevile aliwashukuru Watanzania kwa upendo waliomuonyesha katika kipindi chake pale na kuwahakikishia kuwa angetembea tena.

“Kwa sasa nipo nyumbani Australia, ni kweli tumeachana na Harmonize namtakia kila laheri maishani mwake. Nashukuru kwa wale wote walionisupport nilipokuwa Tanzania na nawapenda wote. Kwa nayo nitarudi kuwatembelea tena. Inshallah,” Briana alisema mwezi Machi.

Ziara yake ya sasa inajiri siku chache tu baada ya Harmonize kumvisha mpenziwe wa sasa Kajala Masanja pete ya uchumba.

Harmonize alipiga hatua hiyo takriban wiki moja iliyopita, kipindi kifupi tu baada ya kurudiana na muigizaji huyo.