"Kim Kardashian aliniiga mtindo, mimi niliuvaa mwaka juzi, yeey kauvaa jana" - Fahyvanny

Fahyvanny aliachana na Rayvanny miaka miwili iliyopita huku Kim Kardashian akiachana na Kanye West miezi sita iliyopita.

Muhtasari

• Wanamitindo hao wawili wana mambo ya kufanana kutoka kuvaa mitindo sawa hadi kuachika katika maahusiano yao na wanamiziki maarufu.

wanamitindo Fahyvanny na Kim Kardashian
wanamitindo Fahyvanny na Kim Kardashian
Image: Instagram

Fahyvanny, mwanamitindo ambaye ni mzazi mwenzake mkurugenzi mkuu wa lebo ya muziki ya Next Level Music, Rayvanny sasa ameibua madai kwamba mtindo wa uvaaji na fasheni ambao mwanamitindo wa marekani Kim Kardashian alitoka nao juzi ni mtindo ambao yeye aliuvaa miaka kadhaa iliyopita.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Fahyvanny alipakia picha yake akiioanisha na ile ya mwanamitindo Kim Kardashian ambapo alisema kwamba mtindo huo wa nywele ndefu wa Kardashian ni mtindo wake alioufikiria na kutoka nao miaka mingi tu iliyopita, na hivyo kuwataka watu wote kuweka heshima wanapotaja jina lake kwani yeye ni mwanzilishi wa mitindo ambayo inaigwa na watu mashuhuri kote duniani.

“Usicheze na #fahyma wewe. Kim kavaa juzi mimi style iyo nilivaa mwaka juzi. LONG HAIR BABE. Kiufupi Kim katuiga jamani,” aliandika Fahyvanny.

Kwenye picha hizo zenye mfanano wa aina yake, Fahyvanny anaonekana kavaa na wigi refu jeusi huku Kardashian kaonekana na wigi kama hilo hilo tu kasoro rangi.

Kwa kuchanganua zaidi, wanamitindo hao wawili wana mambo mengi ambayo wameshabihiana ukiachia mbali uvaaji huo wao wenye mfanano lakini pia kwa njia fulani mahusiano yao ya kimapenzi kama vile yanakaribiana kufanana.

Kwa upande wa Kim Kardashian ambaye ni mwanafasheni na pia mwanasosholaiti mweney umaarufu mkubwa kutokana na kufanya vipindi vya uhalisia kweney runinga za miji ya watu Huko Marekani, miezi michache alitangaza kumalizika kwa ndoa yake ya miaka zaidi ya kumi na mwanamuziki maarufu wa HipHop, Kanye West, jambo ambalo West hakuwa akilitaka kabisa lakini ndio hivo mahakama iliamuru atoe talaka baada ya Kardashian kuelekea mahakamani kutaka ndoa hiyo kuvunjwa.

Kwa upande wa Fahyvanny, pia naye miaka michache iliyopita alitangaza kumalizika kwa ndoa yake na mwanamuziki maarufu ukanda wa Afrika mashariki, mkurugenzi mkuu wa rekodi lebo ya Next level Music, Rayvanny baada ya kukaa kwenye mahusiano na mpaka kujaliwa mtoto mmoja.

Kwa maana hiyo ni sahihi kuchanganua kwamba kando na kuigana katika mitindo, pia katika uhalisia wa maisha, wawili hao hawajaachana sana, katika matendo yote mawili Fahyvanny akiwa ndiye mwanzilishi na Kardashian kufuata.