Huddah awakosoa wanawake wanaoenda kujivinjari vilabuni baada ya kujifungua

Huddah alisema hilo ni thibitisho kuwa mama huyo hana mapenzi ya dhati kwa mtoto wake.

Muhtasari

•Kulingana na Huddah, hilo ni thibitisho kuwa  mama huyo  hana mapenzi  ya dhati  kwa mtoto wake mchanga.

•Huddah pia aliwashauri wasichana kuwa makini  na wanaume ambao wanaoshiriki tendo la ndoa nao.

Mwanasosholaiti Huddah Monroe
Mwanasosholaiti Huddah Monroe
Image: INSTAGRAM

Mwanasoshalaiti Huddah Monroe amewakashifu kina mama wadogo ambao wanaenda kujivinjari katika vilabu  miezi michache tu baada ya kujifungua.

Kulingana na Huddah, hilo ni thibitisho kuwa  mama huyo  hana mapenzi  ya dhati  kwa mtoto wake mchanga.

Huddah alidai kwamba sababu pekee inayoweza kufanya mwanamke aliye na mtoto  kupatikana katika kilabu ni ikiwa anafanya kazi pale au kuuza bidhaa  mle ndani kwa mnajili ya  kujipa kipato cha kulea mtoto  wake.

''Coz Chille jinsi watu wanavyozaa na kukimbilia vilabu inashangaza. Pata mtoto kama uko tayari kulea na kuonyesha mtoto mapenzi ya dhati,mnawawacha na akina  nani ?'' Huddah aliuliza.

Huddah pia aliwashauri wasichana kuwa makini  na wanaume ambao wanaoshiriki tendo la ndoa nao kwani baadhi yao hawapendi kuwajibika pindi wanapopachika mimba.

''Inafaa ujilinde vizuri inapofika katika maswala ya kimapenzi, makahaba ndo hawajali kujilinda anatoka na kila mtu, kama wewe ni mmoja wao  na hiyo ndo namna unapata riziki yako  basi tutakuelewa, lakini jilinde usipate mtoto mapema''Huddah alisema.

Mwanasosholaiti huyo amebainisha kuwa haapendi kuona watoto wakihangaika na hataki mama yeyote kumdharau mtoto wake.