Waliokuwa wapenzi wa Rayvanny walaumiwa kwa kutompongeza akiondoka WCB

Fayvanny na Paula wote waliwahi kuwa wapenzi wa Rayvanny, ambapo tayari msanii huyo ana mtoto na Fahyvanny.

Muhtasari

• "Wanaume tuangalie watu tunazaa nao" wanaume washauriwa baada ya wapenzi wa Rayvanny kukaa kimya kutompongeza.

Msanii Rayvanny na waliokuwa wapenzi wake Fayvanny na Paula Kajala
Msanii Rayvanny na waliokuwa wapenzi wake Fayvanny na Paula Kajala
Image: Instagram

Huku watu mbali mbali wakiendelea kuachia maoni na hisia zao kuhusu msanii Rayvanny kuiaga lebo ya Wasafi rasmi baada ya miaka 6, macho sasa yanaelekezwa kwa waliokuwa wapenzi wake Fahyvanny na Paula Kajala kama watatoa japo neno la kumpongeza kwa kuwa mkurugenzi huru kutoka kwa usimamizi wa WCB.

Maoni yanazidi kutolewa mitandaoni, haswa Fahyvanny akizidi kulaumiwa pakuwa kwa kimya chake licha ya mzazi mwenziwe kupiga hatua kubwa kimaisha.

Baadhi wanahisi wawili hao hata kama ni chuki, wanafaa angalau kuachia tamko la kongole kwa Rayvanny kwa sababu si jambo rahisi mtu kujisimamia mwenyewe kuwa na lebo yake kwa kuanzia kutoka chini bila chochote.

Fahyma, ambaye walizaa mtoto mmoja wa kiume na msanii huyo inasemekana ndiye anayemiliki akaunti za mitandao za mtoto huyo ambapo katika matukio mbali mbali amekuwa akiitumia kumpakia Rayvanny, kwa mfano kama siku ya kina baba duniani, akaunti hiyo ya mtoto ilimtakia kheri njema Rayvanny huku kila mtu akijua fika kwamba huyo ni Fahyvanny alipakia kwa sababu ndiye anamiliki akaunti na mtoto ni mdogo hawezi jua kuitumia.

Sasa mashabiki wanauliza wakati wa tukio kubwa kama hili, panashindikana nini ambacho ni zaidi ya siku moja sasa na akaunti ya mtoto hata haijampongeza babake kwa hatua ya ujasiri wa kuwa na udhubutu wa kujitawala?

Yaani Fahyvanny kwa kitendo cha kukaa kimya maanake amupotezea hata uongozi wa WCB Wasafi ambao ulimkuza na kumlea msanii huyo mpaka wakaja kujuana na kuzaa mtoto pamoja. Mdau mmoja anahisi mwanamama huyo anakosa heshima na kushauri wanaume kuangalia wanawake wanaoingia katika ndoa nao kwani wengine hawawezi kukutakia kila la kheri wakati wa hatua kubwa kama hiyo.

Tena kama Fahyvanny ndio wa kulaumiwa zaidi, yeye ndio anacontrol account ya kile kitoto cha Rayvanny, sasa ameshindwa kupost kule, kitoto kimuwish Mema baba yake, mbona siku ya baba Duniani Kitoto kilimpost Rayvanny, sasa kwenye hili suala Fahyvanny anafeli wapi? Muda mwingine tuwe tunaangalia wake wa kuzaa nao. Fahyvanny ameshindwa kuishukuru hata WCB? Maana bila Wasafi asingekutana na Rayvanny na asingekuwa na umaarufu aliokuwa nao sasa,” aliandika mchangiaji mmoja kweney tasnia ya Sanaa nchini Tanzania.

Je, unahisi ni haki kwa wapenzi wa Rayvanny kulivumbia macho suala hili ama ni vyema wajiunge na wenzao kumpongeza kwa hatua hiyo kubwa ya kufanya udhubutu wa kujisimamia kimaisha?