(Video) Mchungaji amvisha pete ya uchumba mwanamke katika mazishi ya babake

Mazishi yalikuwa na babake mwanadada huyo na mchungaji alikuwa mpenzi wake ambaye alikuja kuhudhuria.

Muhtasari

• Video hiyo iliyopakiwa TikTok ilizua maoni kinzani baadhi wakidai mchungaji angetulia mazishi yaishe kabla ya kuposa.

Katika video ambayo ilipakiwa kwenye mtandao wa TikTok, mwanaume mmoja ambaye alisemekana kuwa ni mchungaji alionekana akimposa na kumvisha pete mwaandada mmoja katika ibada ya mazishi ya babake mwanamke huyo.

Katika klipu hiyo yenye utata, binti wa marehemu ambaye hakutajwa jina anaonekana akilia kwenye mstari wa mbele karibu na jeneza la babake. Kisha, ghafla, mwanaume huyo mchungaji akapiga goti mbele ya dada aliyefiwa akiwa na kipaza sauti na kuuliza swali, na kuwafanya waombolezaji wengine kulia kwa mshtuko. Klipu hiyo inaisha kwa mchungaji kumvisha mpenziwe pete kidoleni, pete ambayo anaonekana kuikubali.

Mchungaji huyo anaonekana kumshukuru Mungu haswa kwa kuwa katika maisha ya mpenzi wake wakati wa wakati mgumu kama huo. Pia alisema kuwa anatumai pendekezo lake litamsaidia kukubaliana na kifo cha baba yake.

Video hiyo ilizua mjadala mkali sana katika mitandao ya kijamii ambapo video hiyo ya TikTok ilisambazwa na watu kuwa na maoni kinzani.

Video ya pendekezo hilo ina maoni zaidi ya laki tatu huku wakosoaji wakimshutumu mwanamume huyo kwa kufanya hafla hiyo ya kusikitisha juu yake mwenyewe.

"Kupendekeza [kwa] binti wa marehemu wakati wa mazishi. Kufuta machozi huko na huko,” inasomeka nukuu ya klipu hiyo, ambayo ilipakiwa wiki kadhaa ziliyopita na mchumba huyo - ambaye anaenda kwa @M.Mojela kwenye TikTok.