logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(Video) Mwanaume avuruta gari kwa kutumia meno

Video hiyo ilirekodiwa maeneo ya Zimmerman, Githurai jijini Nairobi na inamuonesha mwanaume huyo akivuta gari kwa kutumia meno yake.

image
na Radio Jambo

Habari21 July 2022 - 07:42

Muhtasari


• Baadhi walipinga video hiyo wakitaka kamera iangazie usukani kama kuna dereva analiendesha gari kinyumenyume wakidanganya ni meno ya mwanaume huyo yanalivuruta.

Mwanaume mmoja maeneo ya Zimmerman jijini Nairobi amewashangaza wengi kama kile kinachoonekana kweney video ambayo imesambazwa mitandaoni ni tukio la kweli bila uhariri wa aina yoyote.

Kwenye video hiyo, mwanaume huyo anaonekana akifunga gari Kamba kwa nyuma na kisha kuitia mdomoni ambapo anaiuma ile Kamba kwa nguvu za uzito wa nanga na kisha kuanza kuivuta.

Wengi walioona video ile walistaajabu kitendo hicho na kusema huenda mwanaume huyo mweney muonekano na maumbile ya wastani kuwa ni Samson kutoka maandiko matakatifu ya Biblia aliyekuwa na nguvu za kupitiliza mpaka kumuua simba kulingana na maandiko hayo.

Wengi walioiona video hiyo kweney mitandao waliachia maoni yao huku baadhi wakihisi ni miyeyusho na vimbwanga kutokana na ulevi na wengine wakisema huenda bwana huyo ana uraibu wa kutizama filamu nyingi haswa zile zinazotafsiriwa na DJ Afro humu nchini.

“Nadhani huyu anqa uraibu wa kutazama sinema nyingi. Jinsi anavyozungusha mguu wake kana kwamba yeye ni gwiji mdogo,” mmoja aliandika.

Wengine walisema ni uongo mtu hawezi ivuta gari kwa kutumia meno na kutaka waoneshwe upande wa usukani kama kulikuwepo na dereva aliyesaidia kuendesha gari kinyumenyume huku huyo bwana akijifanya ni yeye analivuruta.

“Tuonyeshe kiti cha dereva kwanza. Mnatuekea gari mwendo wa kinyumenyume mnakuja kujichocha hapa nilikuwa mahali hapo wakati wa mitikasi hiyo ya wash wash,” mmoja aliteta.

Maeneo ya Zimmerman yako katika eneo pana la Githurai, eneo ambalo limekuwa likihusishwa kwa muda mrefu na dhana kwamba vitu vyote vinavyopatikana kule ni bandia na vya kughushiwa. Mmoja alisema kwamba katika eneo hilo, kila kitu kinawezekana.

“Ningeshangaa ingekuwa Buruburu. Huko Githurai, kitu pekee ambacho huwezi kupata ni Yesu na Mungu mwenyewe,” shabiki mwingine kwa jina Auncle Felix.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved