(Video) Mwendesha bodaboda aogeshwa baada ya kukwepa maji kwa miaka 3

Mwendesha bodaboda huyo alikuwa hajaonana na maji kwa miaka mitatu mtawalia.

Muhtasari

• Watu walitofautiana kwa kitendo hicho baadhi wakihisi hakufaa kulazimishwa kuoga na wengine wakipongeza kuogesha ja lazima.

Mwanaume mmoja mwendesha boda boda ambaye alikuwa anasemekana hajakoga mwili wake kwa siku nyingi alilazimishinwa kuoga mchana people mbele ya kadamnasi.

Katika video hiyo ambayo ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, mwendesha boda boda huyo kijana anaonekana kuviziwa na wenziwe waliokuwa wamejiandaa vilivyo na maji na sabuni, anajaribu kukataa lakini nguvu za watu wengi waliomzingira zinamzidia na kuoshwa kwa nguvu.

Sauti ya mtu mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wanamuosha anasikika akielezea sababu zilizowafanya wana boda boda wengine kuungana ili kutekeleza kitendo hicho cha aibu lakini chenye stara kwa mwenzao.

“Hapendi kuoga, hajawahi kuoga kwa miaka mitatu sasa. Huyu sasa atakuwa mtu wa aina gani? Harufu karibu na yeye peke inatosha kumhukumu ila kwa leo akubali asikibali, atake asitake, apinga akatae lazima atapaka muosha safi tu,” mmoja anasikika akitoa maelezo.

Watu walionekana kukinzana kwa maoni huku wengine wakisifia kitendo hicho na wengine wakipinga kwani watu hao hawakuwa wanajua sababu za mtu huyo kukataa kuonana na maji kwa muda huo wote.

“Je, itakuwaje mkimuua baada ya kumfanyia jambo hilo la kumuosha, mnajua kweli sababu zake za kutooga kwa miaka hiyo yote?” mmoja kwa jina Mettle Junior alisema.

“Sanduku la mapendekezo ya wateja lilikuwa limejaa😂😂. Kwa ombi maarufu, ikabidi wenzake wachukue hatua ya kulitakaza jina lao kwa wahudumu wa boda boda kwa jumla,” mwingine alionekana kupongeza kitendo hicho.

Video hii inazuka wakati ambapo humu nchini Wakenya wanazidi kutaniana kutokana na hali ya kijibaridi cha mwezi Julai ambapo baadhi wanasema hakuna haja ya kuoga kwani maji ni ya kupika ugali na mchuzi tu. Lakini angalau kwao ni kwa muda tu chini ya mwezi mmoja, hebu tafakari huyu bwana amekaa kwa miezi zaidi ya 36 bila kuonana na maji, na muda huo wote amekuwa akihudumia wateja wanaoabiri boda boda!