Mwanaume aliyeteketeza mkewe hadi kufa, ahukumiwa kunyongwa

Mwanaume huyo aliteketeza mkewe hadi kufa huku akirekodi tukio hilo moja kwa moja kwenye TikTok yake.

Muhtasari

• Tang Lu aligonga vichwa vya habari mwaka 2020 baada ya kurekodi video ya mubashara kwenye TikTok akimchoma mkewe kwa moto hadi kufa.

Lamu, mwanamke aliyeteketezwa hadi kufa
Lamu, mwanamke aliyeteketezwa hadi kufa
Image: BBC

Tang Lu, ni mwanaume mmoja raia wa Uchina ambaye mwaka wa 2020 aligonga vichwa vya habari baada ya kumuua mkewe kwa kumteketeza kwa moto hadi kufa huku tukio hilo akilirekodi mubashara kwenye ukurasa wake wa TikTok.

Mwanaume huyo alishikiliwa na kesi yake imekuwa ikiendelea tangu nyakati hizo ambapo wikend iliyopita majarida mbalimbali duniani yaliripoti kwamba hatimaye kesi hiyo imeamliwa kwa mwanaume huyo kuhukumiwa kunyongwa.

Kwa mujibu wa amri ya mahakama ya Watu wa Juu, Tang Lu alinyongwa siku ya Jumamosi baada ya kupewa hukumu ya kifo kwa mauaji ya kukusudia mnamo2020 ambayo yalizua ghadhabu ya kitaifa.

Kulingana na hati ya mahakamani iliyopakiwa na majarida mengi wikendi, mahakama ilisema kwamba tukio alilolifanya kwa mpenzi wake lilikuwa tukio la kinyama na hivyo alistahili adhabu kali kama hiyo ya kunyongwa.

Lu na mkewe Lamu walitengana mnamo Juni 2020 baada ya miaka kumi na moja pamoja. Wote wawili walifanya kazi kama washawishi kwenye Douyin, toleo la Kichina la TikTok.

Kulingana na maelezo ya awali kutoka kwa mahakama, Lu hakuwa tayari kupata talaka na alijaribu mara kwa mara kurejesha ndoa, lakini Lamu alikataa wazo hilo.

Baadqa ya video ile ya kinyama kuonekana kabla ya kufutiliwa mbali na mamlaka ya mtandao huo unakuja kwa kasi za ajabu, kote duniani watu walizua mjadala mkali kuhusu dhuluma na unyanyasaji wa kinyumbani chini ya alama ya reli Lhamo Act huku wakitaka waathiriwa wa visa vya unyanyasaji katika ndoa kuruhusiwa kuchukua talaka na kujiendea zao badala ya kuwafanyia vitendo vya kinyama kama kile cha kuteketezwa moto.