"Kabla sijafa nataka kukutana na Eminem" - Nikki Mbishi

Madee alimpongeza kwa ndoto hiyo na kumtakia kila la kheri katika kujaribu kuitimiza.

Muhtasari

• “Mungu Akubaliki Champ Mafanikio Siyo Utajili ....Bali Kutimiza Ndoto.... #HoldOn,” shabiki" shabiki mmoja alimhimiza.

Wasanii wa kuchana mistari, Eminem kutoka marekani na Nikki Mbishi kutoka Tanzania
Wasanii wa kuchana mistari, Eminem kutoka marekani na Nikki Mbishi kutoka Tanzania
Image: Instagram//Eminem, NikkiMbishi999

Staa wa zamani wa kuchana mistari ya Hip Hop na rap kutokea Tanzania, Nikki Mbishi amezua maoni kinzani kwenye mtandao wa Instagram baada ya kudai kwamba kabla hajafa anatamani sana kukutana na gwiji wa kuchana mistari kutoka Marekani, Eminem.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nikki Mbishi alisema kwamab kwa muda mrefu sana amekuwa akitaka kukutana na Eminem na ndoto yake hiyo bado ipo pale pale inshallah kabla hajatangulia mbele za haki basi anataka kukutana na msanii huyo kwa kile alisema kwamab ana mazungumzo marefu sana na yeye iwapo atakutana naye.

“Kabla sijafa, ninataka nikutane na huyu mwanaume, nina mazungumzo marefu sana na yeye,” Nikki Mbishi aliandika kwenye picha ya msanii Eminem ambayo alipakia Instagram yake.

Watu mbali mbali walibaki kwenye njia panda wasijue Mbishi ni mazungumzo ani haya marefu ambayo anatamani kwa udi na uvumba kukutana na mwamba huyo wa Marekani kuzungumza naye.

Wasanii wenzake walioanza gemu la kutema madini ya mistari walimpongeza kwa kuwa na ndoto kama hiyo ya kukutana na Eminem na wakamuombea dua kwamba ataifanikisha ndoto yake kabla ya kuenda jongomeo alivyodai.

“Hakuna kinachoshindikana Unju,” msanii Madee alimpa moyo kwa kumuita jina lake la kiutani la ‘Unju’

“Mungu Akubaliki Champ Mafanikio Siyo Utajili ....Bali Kutimiza Ndoto.... #HoldOn,” shabiki mwingine kwa jina Amk Hussle aliandika.

Wengine walimtaka msanii huyo mkongwe kuzidi kuachia mistari kwani amekaa muda hajafanya hivyo na hapaonekani kutokea msanii mwingine wa kuchukua bukta zake kujitoma ulingoni huku wengine wakizua utani kwamab akikutana na Eminem basi ataanza kutema mistari kwa Kiingereza tupu kwa sababu msanii huyo wa Marekani hana kamusi ya kujua Kiswahili.