Aliyeua mwanamke kwa kumkatalia kimapenzi ahukumiwa kunyongwa mubashara runingani

Mohammed Adel mweney umri wa miaka 21 alipatikana na hatia ya kumuua binti Naira Ashraf baada ya kumkataa kimapenzi.

Muhtasari

• Mahakama iliitaka bunge kuruhusu hukumu hiyo ya kunyongwa kupeperushwa moja kwa moja kwenye runinga ya kitaifa.

Kamba ya kujiua
Kamba ya kujiua
Image: Image: Courtesy

Wiki jana, hukumu moja nchini Misri iligonga vichwa vya habari kote ulimwenguni baada ya mahakama kutoa hukumu kwamab jamaa mmoja kwa jina Mohammed Adel anyongwe hadharani tena mubashara runigani kutokana na kupatikana na hatia ya kumuua binti Naira Ashraf aliyemkataa baada ya kumtongoza.

Inasemekana Mshtakiwa Adel alimdunga kisu Ashraf mara 19 na kumchinja huku akijaribu kumkata kichwa.

Mahakama ilitaka mamlaka kuruhusu hukumu hiyo ya kunyongwa kupeperushwa moja kwa moja kupitia runinga ya kitaifa kaam njia moja ya kufikia zuio la jumla linalotarajiwa baada ya kutokea tena na kuenezwa kwa matukio ya kuchinja, jambo ambalo linazua hofu kwa wananchi nchini humo.

Pia mahakama ilijibu ombi la wakili wa utetezi kuwasilisha mshtakiwa kwa dawa ya uchunguzi, kuangalia afya yake ya akili na usawa wa kisaikolojia wakati wa kutenda uhalifu.

Mahakama ilisema kwamba ilitambua uthabiti wa hali yake ya kiakili na kisaikolojia, na utimamu wa ufahamu wake na chaguo lake, kabla na wakati wa kufanya uhalifu wa kumuua mhasiriwa na matokeo yake.

Ilisema kuwa mahakama ilifikia uthibitisho huo kupitia upangaji wa mshtakiwa wa uhalifu huo na uteuzi wa zana ya kutenda uhalifu huo na tarehe na mahali pa kutekelezwa.

Mahakama ya Jinai ya Mansoura mnamo Julai 6 ilisoma hukumu yake dhidi ya mauaji ya Ashraf, baada ya kipindi kifupi sana cha kesi ya kihistoria. Mahakama mnamo Jumanne Juni 28 ilimhukumu Mohamed Adel kifo kwa kunyongwa.

Jumapili, Juni 26, mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo, akidai alilazimika kujitetea baada ya kuonekana kutishiwa na majambazi waliokuwa wakimfuata ili kumdhuru.

Alidai alileta kisu siku ya uhalifu ili kujitetea, na kumshambulia mwathiriwa baada ya kumtusi na kukataa ombi lake la kutaka kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na yeye.

Tukio la mauaji ya mwanafunzi Naira lilisambaa kupitia video katika mitandao ya kijamii na kuzua hasira nchini humo huku mamlaka zikilaumiwa kwa kuchukua hatua kali dhidi ya vitendo vya kiunyanyasaji dhidi ya wanawake.

Shirika la Amnesty International lilitoa ripoti mwaka jana kwamba polisi nchini Misri kutochunguza kutosha unyanyasaji wa kingono na kijinsia kwa wanawake na mahakama hazitoi adhabu ya kutosha.