"Wakristu mtoke mpige kura, msiache wenye dhambi wawachagulie viongozi" - Askofu Ng'ang'a

Alisema Mungu hawezi shuka kuja kuchagua viongozi bali watu ndio watachagua viongozi kulingana na muongozo wa Mungu.

Muhtasari

• “Ningetaka kuwasihi wakristu, msichaguane na mdomo, muende kwa vituo vya kupiga kura na kupanga foleni" - Askofu Harrison Ngang'a.

Kanisa
Kanisa
Image: BIBLE STUDY TOOLS

Askofu mkuu wa kanisa la Christian Foundation Fellowship, Harrison Ng’ang’a wikendi iliyopita aliwazomea wakristu kwa kile alisema kwamba wana hulka ya kukwepa kushiriki katika kuchagua viongozi na badala yake wanaacha wenye dhambi kuwachagulia viongozi ambao mwisho wa siku wanahabribu uongozi na kuanza kuwahukumu.

Ng’ang’a aliwataka Wakristu wote kuweka nadhiri ya kurauka alfajiri na mapema siku ya uchaguzi na kupanga foleni ili kuwachagua viongozi wanaowataka, kwani Mungu hawezi shuka kutoka mbinguni na kuja kuwachagulia viongozi bali ni wao watachagua viongozi kulingana na jinsi roho wa Bwana atakavyowaongoza.

“Ningetaka kuwasihi wakristu, msichaguane na mdomo, muende kwa vituo vya kupiga kura na kupanga foleni. Mkikosa Kwenda kupiga kura wenye dhambi utawaona hapo alfajiri ya saa kumi na mbili hivi wamepanga mlolongo wakiongea vile wanataka na wewe uko kwa kitanda unasema eti Mungu nachukua udhibiti na mamlaka,” askofu Ng’ang’a alisemA.

Pia mhubiri huyo alisema kwamba huwezi ukasema unachukua udhibiti kutoka kitandani mwako bali kufanya hivo ni kuenda kwa kituo mwenyewe na kumchagua kiongozi unayemtaka.

Kulingana na askofu Ng’ang’a, huwezi taka Mungu adanganye eti usiende kupiga kura na mtu mwingine akipiga kura Mungu adanganye kwa kufuta alama za uchaguzi kwa kiroho.

Vile vile, mchungaji huyo alisema kwamba shida inatokea wakati kiongozi ambaye mkiristu amechagua anashindwa, na kuwataka watu kukubali kwamba hata yule ambaye walichagua akishindwa basi wajue ndio matakwa ya Bwana kwamba si yeye aliyefaa wadhfa huo wa uongozi.

“Ni vizuri tuwe waelewa kwamba hata huyu nimechagua akishindwa basi ilikuwa ni mipango ya Mungu kwa yule mwingine kushinda. Usiwe na majungu halafu uanze kusema Baba Mungu mabaya kwa huyu, hakuna haja,” alisema askofu Ng’ang’a.