Ujumbe wa Amber Ray kuhusu maisha yake ya awali wazua gumzo

Amber kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amesema kuwa anafurahia maisha ambayo anaishi kwa sasa.

Muhtasari
  • Kulingana na Amber awali alimuasi Mungu, na kuwakosea wengi bali hayo hayamzuii kuishi maisha yake ya sasa
Amber Ray
Image: Kwa Hisani

Mwanasosholaiti Faith Makau almaarufu Amber Ray amzua gumzo tena mitandaoni baaada ya kusimulia maisha yake ya awali.

Kulingana na Amber awali alimuasi Mungu, na kuwakosea wengi bali hayo hayamzuii kuishi maisha yake ya sasa.

Pia alifichua kwamba alifanya makosa ambayo aliomba msamaha, lakini  makosa yake ambayo alijifunza kwayo ndio yanamfanya aishi maisha yake.

Amber kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amesema kuwa anafurahia maisha ambayo anaishi kwa sasa.

"Kitu ambacho siwezi kuwa na aibu nacho ni maisha yangu ya nyuma... nakubali nimefanya makosa mengi sana, nimevunja sheria nyingi sana, nikamuasi Mungu kwa njia nyingi na kuomba msamaha lakini siwezi kujizuia na maisha yangu ya nyuma coz ndivyo ilivyo. ilinifanya niwe hivi leo ā€¦sijui siku zijazo zimeniwekea nini lakini najua nyasi huwa kijani kibichi kila mara upande ule mwingine; na niko nafurahia sana awamu hii na siwezi kusubiri kuona ukuaji zaidišŸ„° Asante mpenzi wangu kwa kukusudia."