"Waweke mbali nami na binti yangu!" Mulamwah amuonya Sonnie baada ya kutambulisha mpenzi mpya

Mulamwah alimshtumuSonnie kwa kuchumbiana na mzee wa miaka 60 aliye kwenye ndoa nyingine tayari.

Muhtasari

•Mulamwah amemtaka mzazi huyo mwenzake kudumisha heshima hata unapojitosa kwenye mahusiano mengine.

•Mulamwah pia Muthoni  kwa kuchumbiana na mzee wa miaka 60 aliye kwenye ndoa nyingine tayari.

Image: INSTAGRAM/CAROL SONNIE

Mchekeshaji David Oyando almaarufu Mulamwah amemuonya aliyekuwa mpenzi wake Caroline Muthoni dhidi ya kuruhusu mahusiano yake mapya kutatiza uhusiano wake na binti yao Keilah Oyando.

Mulamwah amemtaka mzazi huyo mwenzake kudumisha heshima hata unapojitosa kwenye mahusiano mengine.

"Kuwa na heshima, chumbiana na mtu yeyote unayetaka, bora uwaweke mbali na njia ya msichana huyo mdogo na yangu!" Mulamwah alimwandikia mpenziwe wa zamani kupitia  Instagram.

Baba huyo wa mtoto mmoja alimshtumu Muthoni kwa kumnyima yeye na wazazi wake nafasi ya kumuona binti wao.

"Mtoto ...... ndio unajifanya saa hizi vile unampenda, unaninyima hata mimi wakati wa mtoto na wazazi wangu ati mkaishi kwa wazee? Na huku nje unarant husaidiwi. Kama wewe unafanywa hivo na mtoto mdogo wa kike atafanywaje?" Alisema. 

Mulamwah pia alimshtumu muigizaji huyo kwa kuchumbiana na mzee wa miaka 60 aliye kwenye ndoa nyingine tayari.

Alichapisha picha kadhaa za mpenzi huyo wake wa zamani na kutoa maelezo ya kuyapa nguvu madai yake.

"Mnakulana na wazee wa miaka 60 halafu mnakuja kuset standards kwa mtandao na picha za kipuzi na mahojiano ya kupuzi,"

Baadae aliibua madai kuwa 'mzee' ambaye mzazi  huyo mwenzake anachumbiana naye anatishia maisha yake.

Siku za hivi majuzi hata hivyo amekuwa akijigamba kuhusu mahusiano mapya na kumuonyesha  mpenzi wake wa sasa hadharani. Sonnie hata hivyo amekuwa akionyesha sehemu tu ya mpenziwe na kuficha sura yake.

Katika mahojiano ya hivi majuzi na Nicholas Kioko, Muthoni alidai kuwa ataandaa karamu ya kufichua sura ya mpenzi wake katika siku zijazo.

"Niliamua na kusema wacha watu waone niko na furaha lakini wasione ni nani anafanya niwe na furaha. Hawahitaji kuona uso wake lakini niko na furaha sana," Alisema Sonnie.

Sonnie alifichua kuwa amekuwa akichumbiana na mpenziwe mpya kwa kipindi cha takriban miezi miwili tu.

Hata hivyo alidokeza kuwa yeye na  mpenzi huyo wake mpya wamekuwa marafiki kwa muda mrefu.

"Tumekuwa marafiki kwa zaidi ya miaka 10. Alikuwa nje ya nchi, alirudi miezi michache iliyopita," Alisema.

Katika mahojiano hayo Muthoni pia alikana madai kwamba amekuwa akimnyima mchekeshaji huyo nafasi ya kumuona binti yao Keilah Oyando.

Pia aliweka wazi kuwa hana tatizo lolote na baba wa bintiye, Mulamwa.

"Keilah Oyando anaendelea vizuri kabisa. Mimi na baba yake  hatuna shida yoyote. Wako huru kuonana kwa wakati wowote (Mulamwah na Keilah," Sonnie alisema katika mahojiano na Nicholas Kioko.