Muuguzi wa Kenya akufa maji katika kipindi cha moja kwa moja kwenye Facebook

Dakika 10 pekee kwenye kipindi hicho alianza kupiga mayowe na kujaribu kutafuta hewa.

Muhtasari

•Hellen Wendy anaripotiwa kufa maji wakati wa kipindi cha moja kwa moja ya kwenye mtandao wa Facebook Alhamisi jioni.

•Alikuwa akiogelea kidogo kisha anarudi karibu na  simu yake na kuwajulia hali watu waliokuwa wakimtazama. 

•Wendy aliogelea kwa sekunde chache zaidi kabla ya kuanza kupiga mayowe na kujaribu kutafuta hewa katika dakika ya kumi na sekunde 30.

Image: FACEBOOK// HELLEN WENDY

Muuguzi mmoja kutoka Kenya anayeishi Canada anaripotiwa kufa maji wakati wa kipindi cha moja kwa moja ya kwenye mtandao wa Facebook jana jioni.

Hellen Wendy alianzisha kipindi cha moja kwa moja Alhamisi mwendo wa saa tatu usiku, masaa ya Afrika Mashariki.

Katika kipindi hicho, Wendy ambaye alionekana mchangamfu alijirekodi akijivinjari kwenye bwawa la maji. Hakuna mtu mwingine yeyote aliyeonekana karibu na bwawa hilo.

"Mambo vipi hapo. Mko aje? Eti unalala saa hii? Ni saa nane mchana hapa. Nimetoka kazini. Niko poa. Najibamba tu. Maji ni baridi," Wendy alisikika akiwaambia watazamaji wake mwanzoni mwa kipindi hicho.

Mwanzoni mwa kipindi, Wendy alionekana kuchangamka sana na alionekana kufurahia  kuogelea kwenye bwawa.

Kisha alikuwa akiogelea kidogo na kisha kurudi kwenye simu yake na kuangalia watu waliokuwa wakitazama.

Alikuwa akiogelea kidogo kisha anarudi karibu na  simu yake na kuwajulia hali watu waliokuwa wakimtazama. 

"Unaendelea aje? Maisha inakupelekaje baada ya UDA kuchukua serikali?" Alisikika akimuuliza mmoja wa watazamaji wake.

"Najibamba. Ni saa nane. Raha duniani. Nafurahia," Wendy alisikika akisema katika dakika ya nane ya kipindi kabla ya kurejea majini.

Katika dakika ya tisa unusu alirejea kuangalia simu yake na kujibu ujumbe wa mtazamaji wake mmoja kisha kuingia tena majini.

Wendy hata hivyo aliogelea kwa sekunde chache zaidi kabla ya kuanza kupiga mayowe na kujaribu kutafuta hewa katika dakika ya kumi na sekunde 30.

Hapo alionekana akijaribu kuogelea nje hadi sekunde chache baada ya dakika ya 11 alipotoweka kwenye skrini. Ni vilio vyake tu hafifu vilivyoweza kusikika hadi sekunde mbili kabla ya dakika ya 11 wakati mlio wake wa mwisho uliposikika.

Kisha mzungu alionekana akiingia kwenye bwawa hilo katika saa ya tatu, dakika ya tisa na kuonekana tena akitoka peke yake katika saa ya tatu, dakika  9 mins na alionekana akitoka peke yake dakika tano baadae.

Wanamitandao wameendelea kuomboleza kifo cha muuguzi huyo na kutuma risala za rambirambi kwa familia.