(+video) Mchungaji awatukana waumini kwa kutomnunulia saa ya mkononi

Aliwaita waumini maskini, watu waliovunjika moyo na waliolaaniwa.

Muhtasari

• Mchungaji wa Kansas City Aliwacharukia waumini akiwaita "maskini, waliovunjika moyo na waliochukizwa"

Mhubiri mmoja nchini Marekani eneo la Kansans amegonga vichwa vya habari baada ya kuonekana kweney video akiwasuta waumini wa kanisa lake katika kile kinachoonekana kama ni kuwazomea kwa kukosa kumnunulia saa ya mkononi.

“Mchungaji wa Kansas City Aliwacharukia waumini akiwaita "maskini, waliovunjika moyo na waliochukizwa" kwa sababu hawakumpa pesa za kutosha kununua saa mpya ambayo amekuwa akitaka,” mwenye kupakia video hiyo aliandika, kuvutia watu wengi kutoa maoni yao.

Katika video ambayo imepakiwa kwenye mitandao kadhaa ya kijamii kote ulimwenguni, mhubiri huyo anaonekana akilalama kwamba waumini wake wana uwezo wa kununulia saa ya Mavado lakini kwake linakuwa jambo gumu na hata kuwaita waumini wenye bei duni ya mitumba.

“Hivi mnaniona sina thamani ya chakula chako kizuri cha McDonald’s? Sina thamani ya pesa zako za Red Lobster? Sistahili kuunganishwa kwako kwa St. John? Ninyi nyote hamwezi kumudu bila namna. Sistahili Louis Vuitton yako? Sina thamani ya Prada yako? Sifai kupewa Gucci yako?" mchungaji huyo sharobaro anaonekana kweney video akitema moto kwa waumini wake kanisani.

Mchungaji huyo anaelezea hasira zake kwamba hasemi hivyo ili waumini wake wasiliheshimu neno bali anataka kuelewa ni nini Mungu anajaribu kusema.

“Acha nishushe mlango niongee na wanangu wa kiume na wa kike wa bei nafuu. Tazama ndivyo ninavyojua wewe bado ni maskini, umevunjika, umechanganyikiwa, na umechukizwa kwa sababu ya jinsi umekuwa ukiniheshimu,” mchungaji alipandwa na mori.

Alisema kwamba anawaita maskini na watu mitumba kutokana na ishara wamekuwa wakimuonesha kupitia zawadi ambazo huwa wanamtolea kanisani.