(+video) Baraka mfululizo! Mwanamke azaa mapacha 4 baada ya kusubiri kwa miaka 7

Mwanamke huyo alikuwa anaomba mapacha 2 ila Mungu akambariki na 4.

Muhtasari

• “Mungu naiomba baraka hii kwa dada yangu ili tushuhudie kuwa wewe ni Mungu na maneno yako lazima yatimie AMEN,” shabiki mmoja aliomba.

Klipu moja ya mama aliyezaa watoto wanne kwa mkupuo baada ya kufanya majaribio ya kupata mtoto angalau hata mmoja kwa miaka 7 bila mafanikio imetia bashasha wana mitandao huku wengi wakiamini kwamba kweli miujiza bado hufanyika kwa wale wanaoamini kwa Imani kubwa.

Katika video hiyo iliyopakiwa ukurasa wa Twitter wa maudhui mbalimbali, manesi wanaonekana wakitoka na watoto hao mapacha wanne ndani ya chumba cha kujifungua kina mama na kuiwavalisha nguo huku baba yao akiwa haamini kabisa baraka hizo zilizotiririka kwa mara moja baada ya kutafuta mtoto kwa miaka 7.

“Hii ni nzuri sana. Baada ya kusubiri kwa miaka 7, aliombea mapacha lakini Mungu alimbariki na watoto wanne. Hongera sana,” klipu hiyo ilifuatishwa kwa maneno hayo ya Imani kuu.

Hilo liliwafurahisha wengi huku wengine wakiwa na Imani muujiza kama huo utawatokea kwa wakati wake Mungu akiridhia na mwingine akimuombea dadake pia kufanikiwa na watoto kama hao ili watoe ushuhuda wa nguvu na uwepo wa Mwenyezi Mungu mweney baraka tele.

“Mungu naiomba baraka hii kwa dada yangu ili tushuhudie kuwa wewe ni Mungu na maneno yako lazima yatimie AMEN,” mwingine aliandika.

“Wow hongera kwao naomba MUNGU amshangaze shangazi yangu hivi karibuni kwa baraka kama hii, Amina,” Shabiki mwingine alimtilia dua shangazi yake ambaye pia amekuwa katika ukame wa kupata mtoto kwa muda.