"Niko na mume bora zaidi duniani!" Kajala ajigamba baada ya kuzawadiwa na Harmonize

Wachumba hao waliadhimisha miezi miwili ya uchumba wao mnamo Agosti 25.

Muhtasari

•Konde Boy  alimkabidhi mpenzi wake zawadi hiyo mmoja mnamo siku ya kuadhimisha uchumba wao.

•Harmonize alionyesha picha iliyodokeza walikuwa na mipango maalum ya kuadhimisha siku ya uchumba wao  

Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Muigizaji Frida Kajala Masanja alishindwa kuzuilia furaha yake baada ya mchumba wake Harmonize kumzawadia mkufu wa thamani.

Konde Boy  alimkabidhi mpenzi wake zawadi hiyo mmoja mnamo siku ya kuadhimisha uchumba wao. Wachumba hao waliadhimisha miezi miwili ya uchumba wao mnamo Agosti 25.

Ili kuonyesha upendo wake kwa Kajala, bosi huyo wa Konde Music Worldwide alimsurprise mchumba huyo wake kwa cheni hiyo ya thamani.

"Niko na mume bora zaidi duniani @harmonize_tz. Shukran hommie," Kajala alisherehekea kupitia ukurasa wake wa Insatagram.

Aliambatanisha ujumbe wake na video iliyoonyesha mkufu huo wa rangi ya dhahabu ambao alikabidhiwa na mchumba wake. 

Kwenye ukurasa wake, Harmonize alionyesha picha iliyodokeza walikuwa na mipango maalum ya kuadhimisha siku ya uchumba wao  

"Kama vile jana usiku. Nakupenda sana bro @Kajalafrida," Aliandika Harmonize.

Mnamo Juni 25, Harmonize alipiga hatua ya kuomba ndoa na Kajala, takriban miezi miwili tu baada yao kurudiana.

Mwezi uliopita staa huyo wa Bongo alimhakikishia ndoa mchumba huyo wake wakati akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Harmonize alimwambia Kajala kwamba kumfanya meneja wa kazi zake za kimuziki ni ishara tosha kuonesha kiasi gani anamkubali, kumuamini na kumpenda bila kujali maneno ya watu kuhusu tofauti kati ya umri wao.

“Kheri njema ya siku yako ya kuzaliwa mpenzi wa maisha yangu MISS BANTU. Kukuoa ni ndoto na nashukuru Mungu tunakaribia hapo. Kukufanya meneja wa kazi zangu za kimuziki inaonesha kiasi gani nakuamini na kiasi gani wewe ni wa muhimu katika maisha yangu. Najua wengi wanakubeza, wengi hawaamini kwamba unaweza simama imara. Katika kazi hii yenye ugumu wake, ndio wewe unaweza,” Alisema kupitia Instagram.

Mwimbaji huyo alitambua kuwa Kajala alimfanya akang’aa tena  wakati maisha yake yalikuwa yanaona kiza kinene mbele na pia kusema kwamba Kajala alimfanya kuwaheshimu wanawake kwa kiasi kikubwa mno