logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Mwalimu mwenye umbile la kupendeza anawachanganya wanafunzi" wazazi wataka afutwe kazi

Baadhi ya wazazi wanadai afukuzwe kazi huku wengine wakisema avae tu nguo zinazoficha maumbile yake.

image
na Radio Jambo

Dakia-udaku27 August 2022 - 10:43

Muhtasari


• Mwalimu huyo ni maarufu sana kwenye Instagram ambapo yeye hupakia mara kwa mara picha zake akiwa darasani na pia akifanya shughuli nyingine za kufurahisha akiwa nje ya shule.

Mwalimu mwenye umbile nene na kiungo chembamba

Mwalimu wa sanaa Kutoka New Jersey Nchini Marekani amejipata katika mzozo mkali na wazazi baada ya wazazi hao kuteta kutokana na umbo lake lenye wanasema linawachachafya wanafunzi darasani.

Mwalimu huyo amekosolewa vikali kwa umbo lake alivyoumbika huku wazazi wakimtuhumu kuwa msumbufu wa akili za wanao.

Umbo lake na mavazi yake ni sababu kubwa kuwa inawafanya mpaka watoto wabaki kumuangalia mwalimu badala ya kupata kile anachokifundisha Darasani, Wazazi walisema umbo lake na muonekano wake ni tatizo kwa watoto wao.

Mwalimu huyo ni maarufu sana kwenye Instagram ambapo yeye hupakia mara kwa mara picha zake akiwa darasani na pia akifanya shughuli nyingine za kufurahisha akiwa nje ya shule.

Baadhi ya wazazi wanadai afukuzwe kazi huku wengine wakisema avae tu nguo zinazoficha maumbile yake.

Chini ya sheria ya New Jersey na sheria ya shirikisho la kazi, itakuwa kinyume cha sheria kwa shule kumfukuza kazi mwalimu kulingana na sura yake, ambayo labda ndiyo sababu na hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi ya malalamiko yanayodaiwa ambayo yametolewa kuhusiana na sura ya mwanamke huyo na umbile lake.

Taarifa hiyo ilichapushwa na majarida na wanablogu wengi kote duniani huku wengi wakivutiwa na umbo la mwalimu huyo na kusema kwamba haina haja ya wazazi kuteta kwani wanafunzi anaowahudumia bado ni wadogo kufikiria mpaka kiwango cha mapenzi.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved