logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+video) Mchungaji Mmarekani mweusi ateta kukamatwa na polisi bila hatia

“Video hii inaweka wazi kuwa maofisa hawa waliamua kumkamata Mchungaji Jennings chini ya dakika tano. Ni ujinga, kutowajibika na kinyume cha sheria,” NPR walimnukuu mwanasheria wake.

image
na Radio Jambo

Habari31 August 2022 - 08:06

Muhtasari


• Mchungaji huyo alikamatwa katika nyumba yake akinyunyizia bustani.

• Polisi wanamkaribia na kumtaka kujitambulisha na baada ya kuzozana wanamtia pingu.

Visa vya watu Weusi kunyanyapaliwa na kubaguliwa kutokana na rangi ya Ngozi yao si jambo geni haswa katika mataifa ya Wazungu.

Jana, shirika la polisi Marekani limeachia mkanda wa video unaonesha jinsi mhubiri mmoja Mmarekani mweusi kwa jina Michael Jennings alitiwa mbaroni na polisi bila makosa.

Katika video hiyo, mhubiri Jennings alionekana akiwa katika boma lake huku akinyunyisia bustani la maua maji kabla ya polisi kumkaribia na kumuuliza maswali na kisha kumlazimisha ndani ya gari lao.

Mkanda huo uliopakiwa na jarida la NPR na ambao mchungaji Jennings anasema kukamatwa kwake kulikuwa bila hatia bali ni ubaguzi wa mara unaonesha polisi wakimtaka kujitambulisha.

Kwa kuamini kwamab hajafanay kosa lolote alikataa kabisa kujitambulisha kwa polisi hao ambao walimsrutisha na kisha akajitambulisha shingo upande. Polisi walimuambia kwamba kuna mtu aliita polisi ili kufika kumkamata.

“Sikufanya chochote kibaya, na, Si lazima nijitambulishe, Napaswa kuwa hapa. Mimi ni Mchungaji Jennings. Ninaishi ng'ambo ya barabara ila kama mnataka kunitia mbaroni, basi nikamateni. Sihitaji kujua nani aliwapigia simu, nyinyi nikamateni ndio tuone nini kitaendelea baadae,” mchungaji huyo anaonekana akiteta huku akilazimishwa ndani ya gari la polisi.

Kulingana na jarida la NPR, mwanasheria aliyekuwa akimwakilisha mchungaji Jennings alisema kwamab kuachiwa kwa klipu hiyo kutatoa fursa nzuri zaidi ya kisheria kwa mteja wake kupata haki.

“Video hii inaweka wazi kuwa maofisa hawa waliamua kumkamata Mchungaji Jennings chini ya dakika tano baada ya kuvuta na kujaribu kuandika upya historia akidai kuwa hajajitambulisha wakati hilo ndilo jambo la kwanza alilofanya, Ni ujinga, kutowajibika na kinyume cha sheria,” NPR walimnukuu mwanasheria huyo.

Video hiyo ilimuonesha pia mwanamke ambaye alisema kwamab ndiye alipigia maafisa wa polisi simu kwa kumshuku Jennings. Baadae anakiri kwamba anamjua na kusema ni kamosa yake ila polisi hao bado wanamtia pingu mchungaji na kuondoka naye.

“Anaishi hapo hapo, na angekuwa anamwagilia maua yao. Hili labda ni kosa langu," jirani huyo anaonekana akikiri kosa lake kwa polisi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved