"Ni mimi na wewe mpaka mwisho!" Njugush amsherehekea mkewe Celestine Ndinda

Mchekeshaji huyo alimshukuru Bi Ndinda kwa kusimama naye na kuamini katika safari yao.

Muhtasari

•Mchekeshaji Njugush hajaachwa nyuma katika kumsherehekea mkewe huku akichukua fursa  kufufua kumbukumbu ya umbali waliotoka.

•Njugsush alimtakia mkewe heri za siku ya kuzaliwa na kuahidi kuwa naye katika siku zote za maisha yao.

Image: INSTAGRAM// BLESSED NJUGUSH

Mtumbuizaji Celestine Ndinda almaarufu Wakavinye anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Mamia ya wanamitandao wamemsherehekea mama huyo wa mtoto mmoja na kumwandikia jumbe za kheri ya siku ya kuzaliwa.

Mchekeshaji Njugush hajaachwa nyuma katika kumsherehekea mkewe huku akichukua fursa  kufufua kumbukumbu ya umbali waliotoka.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Njugush alipakia picha yao iliyopigwa miaka kadhaa iliyopita na kueleza kuwa siku hiyo walikuwa wanaenda kutafuta nyumba yao ya kwanza kuishi pamoja jijini Nairobi.

"Siku hii tulikuwa tunaenda kutafuta nyumba yangu ya kwanza Nairobi ili nihame kwa mathe Joska, Kamulu. Tulipata nyumba pale transami kwa hisani ya mama watoto wangu. Tulipata nyumba ya ghorofa nne ilikua na mabedsitter tupu ... shida yangu kubwa ilikua nitamwaga wapi maji ya sufuria ya ugali.... ushamba ndani yangu nilisomeshwa na wewe @celestinendinda," aliandika chini ya picha hiyo.

Baba huyo wa mtoto mmoja alimshukuru mkewe  kwa kusimama naye na kuamini katika safari ya ndoa yao.

"Ni ya mwendo wa polepole lakini ya kikweli," Alisema.

Aliongeza, "Asante kwa kuwa kweli kila wakati. Daima unaishi wakati huo uwe mzuri au mbaya, tuangalie sasa !!!!!!

Njugsush alimtakia mkewe heri za siku ya kuzaliwa na kuahidi kuwa naye katika siku zote za maisha yao.

"Kheri ya siku ya kuzaliwa  mama wa wanangu. Yani ni mimi na wewe mpaka mwisho," 

Bi Ndinda alimshukuru mumewe kwa ujumbe huo mtamu na kumwagiza kutoa zawadi kwa ajili ya siku hiyo muhimu katika maisha yake.