"Iliisha!" Huddah afunguka kuhusu nia yake halisi na Juma Jux

Mwanasoshalaiti huyo amefichua kuwa huo ulikuwa mradi tu waliokuwa nao pamoja.

Muhtasari

•Wasanii hao walidokeza kuhusu mahusiano ya kimapenzi kati yao kutokana na ukaribu wao na matendo yao pamoja hadharani katika kipindi kile.

•"Kama Raila, Ulikuwa tuu mradi. Na uliisha," alisema katika kipindi cha maswali na majibu kwenye Instagram

Image: INSTAGRAM// JUMA JUX

Hatimaye mwanasoshalaiti mashuhuri Huddah Monroe amefunguka kuhusu uhusiano wake halisi na staa wa Bongo Juma Jux.

Takriban miezi miwili iliyopita, wasanii hao wawili kutoka mataifa ya Afrika Mashariki walidokeza mahusiano ya kimapenzi kati yao kutokana na ukaribu wao na matendo yao pamoja hadharani katika kipindi kile.

Huddah hata hivyo sasa amefichua kuwa huo ulikuwa mradi tu ambao walikuwa nao pamoja na kwa sasa tayari umeisha.

"Kama Raila, Ulikuwa tuu mradi. Na uliisha," alisema katika kipindi cha maswali na majibu alichoshirikisha wafuasi wake kwenye Instagram.

Mwanasoshalaiti huyo kutoka Kenya alikuwa akimjibu shabiki aliyemhojikuhusu hali ya Jux.

Mapema mwaka huu Huddah na Jux waliwakanganya mashabiki wao kuhusu uhusiano wao baada ya kuonekana pamoja mara kwa mara na hata kufanya mambo mbalimbali ambayo yalidokeza wanachumbiana. Wawili hao walionekana wakijivinjari pamoja, wakikumbatiana na hata kupigana busu hadharani.

Katika video moja iliyowaonyesha wakiwa wamebarizi nyumbani kwake Jux, wawili hao hawakuogopa kubusu mbele ya kamera na kuambiana maneno matamu ya kimapenzi. 

"Mimi na mpenzi wangu tumetulia tu.. sijui, ningependa kuwa kitandani na wewe," Huddah alisikika akimwambia Jux.

Haya yalitokea siku chache tu baada ya staa huyo wa Bongo kumshirikisha Huddah katika video ya kibao chake 'Simuachi.'