Mwanaume apeana vitu vya mpenzi wake kama msaada baada ya kumpata akimsaliti

Alichukua vitu vyote na kuvipeana kwa shirika la kutoa msaada wa kibinadamu kwa wat uwasiojiweza

Muhtasari

• Alipomfumania, hakumuambia kitu chochote, alisubiri ameenda safari na rafiki zake naye akavipeana vitu vyote kabla ya kuhamia kusikojulikana.

Mwanaume aliapeana vitu vya mpenzi wake kama msaada
Mwanaume aliapeana vitu vya mpenzi wake kama msaada
Image: Twitter

Bila shaka, tukio moja la kuuma kwa uchungu mno ni kumpata mtu ambaye ulikuwa unamuaminia kwa hali na mali akikugeuka na kukusaliti. Hali huwa ni mbaya zaidi ukipata kwamba ni mtu uliyekuwa umewekeza hisia zako za kimapenzi kwake.

Ndio hadithi ya jamaa mmoja kama ilivyoelezewa kweney mtandao wa Twitter na rafiki yake.

Jamaa huyo ambaye rafiki yake hakumtaja jina alimpata mpenzi wake wa muda mrefu akichepuka na kumsaliti kimapenzi.

Jamaa wa watu baada ya kumpata msichana huyo anamsaliti, hakumwambia wala kumuuliza kitu. Alijifanya kauzu asiyejua be wala te, kumbe kuna mchongo alikuwa anausikilizia uivane!

Alimsubiri mpenzi huyo wake ametoka Kwenda ziara yake ya kawaida na mwanaume aliyekuwa akichepuka naye na jamaa huyo alipanga vitu vyote alivyokuwa amempa mwanadada huyo kama zawadi. Alivichukuwa na kuvitoa kama msaada katika shirika moja la kutoa msaada wa kibinadamu kwa watu wasiojiweza.

Rafiki huyo wake anayejiita Camhoudini alieleza kwamab rafiki yake kwa uchungu na kutamauka, hakuishia hapo bali alienda kwa baba mweney nyumba akaivunja mkataba wake na kuondoka kwenye nyumba nyingine mbali na mtaa huo.

Alielezea kwamba rafiki yake anaondoka Ijumaa hii Kwenda nyumba mpya na wengi walibai na swali la itakuwaje yule mwanadada akirudi wiki ijayo na apate mumewe hayupo kweney nyumba waliokuwa wamepangisha.

“Jirani yangu alimfumania mpenzi wake akichepuka hakuwahi kusema lolote ..alisubiri hadi alipoenda safari na marafiki zake na kutoa vitu vyake vyote kwa shirika la kutoa msaada wa kibinadamu kwa watu wasiojiweza,” alieleza kwenye Twitter.

Aliendeleza hadithi hiyo ya kutia huruma kwamba yeye ndiye alikuwa mstari wa mbele kumsaidia kuvihamisha vitu vyake Kwenda nyumba mpya kwa malipo.

Wengine walimtaka kuendeleza simulizi zaidi siku huyo mwanamke atakaporudi kutoka ziara na kuwaeleza kwenye Twitter jinsi atakavyofanya kwa kupata mumewe hayuko na nyumba ipo chini ya mpangaji mpya kama itakuwa imechukuliwa.