"Ni yote niliyohitaji!" Akothee ajitosa kwenye mahusiano mapya baada ya kutengana na Nelly Oaks

Akothee amekuwa akionyesha mwanaume mzungu na kudokeza kuwa ni mpenziwe mpya.

Muhtasari

•Siku za hivi majuzi mama huyo wa watoto watano amekuwa akionyesha mwanaume mzungu na kudokeza kuwa ni mpenziwe mpya

•Katika chapisho lake la Jumanne Akothee alionyesha picha ya paka wake Orpa akiwa ameficha uso wa mwanaume huyo.

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Mwimbaji Esther Akoth almaarufu Akothee anadaiwa kupata mpenzi mpya  miezi michache tu baada ya kutengana na Nelly Oaks.

Siku za hivi majuzi mama huyo wa watoto watano amekuwa akionyesha mwanaume mzungu na kudokeza kuwa ni mpenziwe mpya. Akothee hata hivyo bado hajaonyesha sura kamili ya mwanaume huyo.

Hivi majuzi kwenye Instagram mwanamuziki huyo alichapisha picha iliyoonyesa akipapasa kichwa cha mzungu huyo na kuambatanisha na ujumbe ambao uliashiria hisia ya mahaba tele kati yao.

"Anapolala kwenye mapaja yangu na kuhisi mapigo ya nyoyo zetu... Ni yote niliyohitaji," aliandika chini ya picha hiyo.

Video nyingine ambayo alipakia kwenye Instagram ilimuonyesha akiwa jikoni pamoja na mwanamume huyo asiyejulikana.

Katika chapisho lake la Jumanne Akothee alionyesha picha ya paka wake Orpa akiwa ameficha uso wa mwanaume huyo.

"Mmm Orpa, nataka ujasiri wako tu kwa sasa, orpa inanikumbusha wale watoto wa kitajiri ambao wangeendesha magari ya kuchezea huko kwenye vichwa vya wageni, zzzzzzzz, zzzzzzzz, na sa hiyo kwao wamepika tu spaghetti 🤦 Orpa acha," Akothee aliandika chini ya picha hiyo.

Baadhi ya wanamitandao ambao walitoa maoni chini ya chapisho hilo walizungumzia hatua  yake kupata mpenzi mpya.

@phelix_angel Huyu ni mume namba ngapi

@unique_zara_collections Mwingine???

@marymetito Nellyoaks wacha akaoe sasa😂

Takriban miezi mitatu iliyopita, msanii huyo mwenye umri wa miaka 42 alithibitisha kutengana kwake na Nelly Oaks baada ya kuchumbiana kwa muda.

Katika taarifa yake kwenye Instagram, Akothee alibainisha kuwa aliamua kukatisha mahusiano hayo na kuzingatia kazi yake na furaha mpya iliyopatikana.

"Nimetoka kwenye mahusiano mengine yenye misukosuko tofauti kwa hivyo hii ya mwisho isiwe ya kushtua au ya kushangaza. Ni uamuzi wa kibinafsi tu, ninahitaji wakati wa kuzingatia furaha yangu mpya iliyopatikana na uharibifu mdogo, ninahitaji kujishughulisha mwenyewe na kazi yangu," alisema.

Mwimbaji huyo aliweka wazi kuwa hakuwa tayari kutoa maelezo zaidi kuhusu kilichovunja mahusiano yake na meneja huyo wake wa zamani.