Shoga Silas Miami amepakia picha akijivinjari Mombasa na mpenzi wake mzungu

Miami ni mtoto wa mtangazaji mkongwe Louis Otieno

Muhtasari

• Silas alipakia picha akiruka juu ya kochi na mbwa huku akitangaza kuwa alikuwa Vipingo Ridge ufukweni.

Shoga Silas Miami na mpenzi wake mzungu
Shoga Silas Miami na mpenzi wake mzungu
Image: Instagram

Silas Miami, shoga ambaye ni mtoto wa mtangazaji mkongwe wa runinga Louis Otieno amepakia picha kadhaa kweney mtandao wake wa Twitter akiashiria kwamba hatimaye ametua nchini Kenya akiandamana na mwanaume mpenzi wake mzungu.

Kupitia msururu wa picha alizopakia kwenye Instagram yake, Miami alionesha akiwa kwenye ndege na mzungu mpenzi wake na baadae akaonesha picha nyingine akiwa kwenye mgahawa maarufu pwani ya Kenya, Vipingi Ridge.

Silas alipakia picha akiruka juu ya kochi na mbwa huku akitangaza kuwa alikuwa Vipingo Ridge ufukweni.

Silas kisha akafichua kwamba mume wake mzungu alikuwa ameambatana naye kwa safari hiyo kwani walionekana wakijumuika na Ciku na marafiki wengine.

“Njoo. Tazama furaha. Je, umewahi kuja hai katika bafuni ndogo? Tafuta watu wako. Pia, Ciru ndiye pekee aliyeelewa mgawo huu,” aliandika katika picha nyingine akiwa na kundi la watu.

Miami aligonga vichwa vya habari miezi michache iliyopita baada ya kutangaza kwamba hawezi kumtambua babake mzazi mzee Louis Otieno kwa kile alisema kwamba babake ndiye alikuwa wa kwanza kumkana na hivyo yeye anafanya marejeleo tu.

Katika mahojiano na mtangazaji wa runinga moja ya humu nchini kipindi hicho, Miami alisema kwamba hawezi kumtambua Otieno kuwa babake hata kwa dawa kwa sababu mzee huyo alisema hamjui kabisa na hakuwa anataka kujihusisha na yeye kwa njia yoyote.

Alisema kwamba babake alianza kujipendekeza kwake pindi tu baada ya mafanikio yake kuanza kung’aa.