(+video) Kina mama wa kanisa walala chali barabarani kuombea amani kwa nchi

Wanawake hao wapatao 40 kutoka kanisa la Methodist walikuwa wanaopa Mungu kuleta amani.

Muhtasari

• Ilielezewa kwamba walikuwa wakifanya sala ya kuomba Mungu kuleta amani baina ya jamii mbili zinazopigana eneo hilo.

Afrika ni bara lililobarikiwa kwa njia tofauti tofauti. Moja ya baraka zilizotundikwa katika bara hili ni uhuru wa kuabudu na madhehebu ya kila aina.

Kila dhehebu lina njia yake ya kipekee ya kuendesha shughuli zake za kuabudu na kumsujudia Mungu.

Nchini Nigeria, kuna video moja imesambazwa mitandaoni ikisemekana kuwa ni ya waumini wa kanisa la Methodist wakiwa wamelala chali barabarani kama njia moja ya kuomba amani.

Video na picha hizo zinawaonesha makumi ya wanawake waliovalia sare za kanisa hilo wakiwa wanajitebweresha kati kati mwa barabara wakidai kwamab ni njia moja ya kumuita Mungu kuingilia kati hali tete ya usalama katika jimbo hilo.

Mmoja wa watumizi wa Twitter aliyeelezea tukio hilo kwa watu waliokuwa hawajui kilichokuwa kikiendelea alisema kwamba kina mama hao waliandamana mpaka makutano ya barabara moja maarufu na kulala chini kwa kile walisema ni kuita Mungu kuleta mapatano ya amani kati ya jamii mbili zinazozozana na kuuana hovyo.

“Wanawake wa Kanisa la Methodist la Nigeria walionekana wakiwa wamelala kwenye sakafu tupu kwenye makutano maarufu ya Orpet kando ya Jimbo la Umudike Umuahia Abia, wakimwomba Mungu aingilie kati masuala ya Jimbo la Abia na kuwaokoa Ikpeazu. Ikpeazu wamemaliza Abia. Kosa kubwa sana,” Von Bismack aliandika kwenye Twitter.

Wengine waliopakia tukio hilo walisema kwamba kina mama hao wa kanisa Methodist walikuwa wanamuita Mungu kudhihirisha uwepo wake katika eneo hilo ambalo wanasema ni la Mungu mwenyewe, huku wengine wakisema walikuwa wanaomba Mungu kuwapa viongozi wema wa kuleta upatanishi wa Amani.