(+video) Mwanamke ateta kupigwa ngumi usoni na mchungaji wakati wa maombi

Wengine walimtania kwamba pengine aliwahi mkosea mchungaji huku wengine wakisema ni kutotoa sadaka.

Muhtasari

• Juzi, mchungaji mmoja kutoka Uganda aligonga vichwa vya habari baada ya kuonekana kwenye video akiwacharaza waumini.

Mwanamke mmoja ameshindwa kuzuia hasira zake baada ya mhubiri mmoja kumuombea kwa kumpiga ngumi kwenye paji la uso.

Katika video iliyopakiwa TikTok, mwanadada huyo anaonekana akiteta vikali kwamba mchungaji huyo alikuwa akimuombea na kumpiga ngumi kwa uchungu usoni kama njia ya kumsukuma kuanguka chini ili kudhihirisha kwamba ameshikwa na roho mtakatifu.

Mwanamke huyo anaeleza kwamba imekuwa mazoea ya mchungaji huyo kumpiga kwa ngumi mpaka macho yake mara nyingine yanapata uvimbe kutokana na maumivu ya ngumi za mchungaji.

Akielezea mtu mwenye alikuwa akirekodi video hiyo, mwanamke huyo anasema mchungaji huwa anapiga watu ngumi usoni kama njia ya kuyaondoa mapepo ndani mwao na kuwatakasa.

"Mchungaji alikuwa anataka kunifanyia utakaso, ananipiga ngumi machoni mpaka macho yangu yanavimba," msichana huyo anaelezea watu wakicheka.

Video hiyo iliibua maoni mseto wengine wakimhurumia na wengine wakimtania.

“Wewe una tofauti za kibinafsi na mchungaji, hawezi kupiga bure,” Jupiter aliandika huku akifuatisha na emoji za kucheka.

“Huwa hutoi sadaka kanisani ndio maana”

“Huyu hayuko makini kuhusu unyanyasaji wa aina hii aliofanyiwa. Inakuwaje alipigwa ngumi usoni wakati wa ibada ya kanisa. Ninaomba alitambue kanisa kwa hatua kali,” mwingine alitolea maoni bila utani.

Wenginecwaliendeleza utani kwamba hilo ni onyo dhidi ya watu wanaofikiria Kwenda kanisani na kufuata kila agizo la mchungaji mpaka lile la kupotosha eti kwa sababu ni mtu wa Mungu.

Itakumbukwa hii si mara ya kwanza wachungaji katika bara la Afrika wanajipata katika mijadala ya mitandaoni baada ya vitendo visivyo vya kawaida.

Juzi, mchungaji mmoja kutoka Uganda aligonga vichwa vya habari baada ya kuonekana kwenye video akiwacharaza waumini eti anawatakasa kwa viboko mgongoni kama upako.