(+video) Kijana arudisha cheti chake cha digrii chuoni, ataka kurudishiwa karo yake

Sababu yake ilikuwa ni kukosa kupata kazi kutumia digrii ile na sasa akitaka pesa zake kuanzisha biashara binafsi.

Muhtasari

• Baadae alipoulizwa sababu zake, alisema alijaribu kutafuta kazi ila akakosa na kuamini kwamab digrii ile haina msaada wowote kwake.

Kijana mmoja amezua mjadala mitandaoni baada ya video yake akizua tafrani katika sehemu ya mapokezi ya chuo alichosomea.

Mwanaume huyo alikuwa akirudisha cheti chake cha shahada katika chuo hicho ili kurejeshewa pesa zote alizozitumia kufadhili masomo yake.

Katika video hiyo, mwanaume huyo mwenye tisheti jeupe anaonekana akizua vikali kwamba masomo aliyoyapata katika chuo hicho hayajamfaidi kivyovyote na ndio maana alitaka kurejeshewa karo yake na chuo kurudisha cheti chao chenye ‘hakina maana’

Video hiyo ilipokelewa kwa njia tofauti huku baadhi wakitumia misemo kumshauri kwamba mtu huwezi ukaila keki yako na bado ukataka kuwa nayo mkononi.

“Kurudisha cheti? Inakuwaje na masomo aliyopata tayari? Atairudisha elimu hiyo pia?” mmoja kwa jina Edwin Silas kwenye Twitter aliuliza.

Baada ya video hiyo kusambaa, watu mbali mbali walimfikia na wengine kutaka kujua ni kwa nini aliamua kuchukua uamuzi kama huo wa kuzua kioja katika chuo chake cha awali.

Katika video nyingine ambayo imepakiwa kweney mtandao wa Instagram, mwanaume huyo alijieleza kwamba kutokana na kutamauka kwa kutafuta kazi bila mafanikio, aliwaza labda cheti hicho ni bure maishani mwake na kuamua kukiridisha ili kufikidwa karo yake akafie mbele.

Alisema kwamba amejaribu juu chini kupata kazi lakini hajafanikiwa na kwamba hawezi jihusisha Katika kazi za ujambazi sababu ndoto yake tangu utotoni ilikuwa kuwa mtu wa maana katika kujenga uchumi wa taifa lake.

Baada ya kujieleza kwa huruma, watu wengi waliokuwa wakimcheka katika video ya awali sasa wamejitolea kuomba namba yake ili kumpa msaada kujikwamua kimaisha.