logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwinjilsti Jennifer Mgendi afichua njia 10 za kumjua rafiki mnafiki

Mkikubaliana mambo ya msingi anajifanya amesahau hasa yale mambo yanayokuhusu wewe ila yake kamwe hayasahau. - Mgendi.

image
na Radio Jambo

Burudani12 September 2022 - 07:51

Muhtasari


• Ukiwepo anakusema vizuri lakini ukimpa mgongo tu anakuponda. - mGENDI.

Mwanamuziki wa injili na muigizaji Jennifer mgendi

Mwimbaji mkongwe wa miziki ya Injili Jennifer Mgendi ameamua kuwatumbua marafiki wa uongo kwa kutolea dalili za kuwajua marafiki wanafiki.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mgendi akidokeza kuachia kibao chake kipya kwa jina Amenivusha hivi karibuni, alitoa vigezo kumi vya kuzingatia ili kumjua rafiki yako kama ni wa kweli ama ni mnafiki.

1. ANAKUTAFUTA AKIWA NA SHIDA TU

Hakutafuti katika mazingira ya kawaida ni mpaka pale anapokuwa na shida yeye. Kwa ufupi amekufanya "spare tyre"

2. ANAKUONGELEA VIBAYA USIPOKUWEPO

Ukiwepo anakusema vizuri lakini ukimpa mgongo tu anakuponda.

3. ANAONEA WIVU MAFANIKIO YAKO

Hafurahii mafanikio yako hasa pale inapoonekana wewe unamzidi kimafanikio anaumia.

4. ANATOA SIRI ZAKO

Unapomshirikisha mambo yako ya ndani anawaambia marafiki zake wengine ili kufanya uonekane si lolote.

5. HUTAMWONA NYAKATI NGUMU

Hutamuona nyakati ngumu anasubiri nyakati za raha zaidi. Hakosi visingizio vya kutopatikana unapomhitaji.

6. HAKUSAMEHI

Ukimkosea hakusamehi upesi na angependa kuvunja urafiki kwa makosa yanayosameheka.

7. HAKUSIKILIZI

Hakusikilizi unapoongea naye anakuwa busy na simu au mambo mengine. Mkiwa na watu wengine ndio kabisa hana mpango na wewe.

8. ANA TABIA YA "KUSAHAU"

Mkikubaliana mambo ya msingi anajifanya amesahau hasa yale mambo yanayokuhusu wewe ila yake kamwe hayasahau.

9. ANAPENDA KUSHINDANA NAWE

Ukinunua kitu fulani kizuri naye anataka, ukimpeleka mwanao shule fulani nzuri naye anataka yaani ni mashindano tu.

10. Jaza.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved