Bosi amfumania kijakazi kwenye kiti chake huku akinywa divai yake kutoka kwa chupa (+video)

Jamaa huyo kijakazi alikuwa anajua bosi hayuko ndipo aliamua kuonja kinywaji chake moja kwa moja kutoka kwa chupa.

Muhtasari

• Watu mbali mbali walijumuika kutolea ushuhuda wao jinsi walivyowafumania wafanyikazi wa ndani wakifanya matukio kwenye nyumba zao.

Jamaa mmoja ambaye ni kijakazi alipatikana na bosi wake akiwa ameketi katika kiti cha bosi wake huku akiibia divai yake na kuibugia mdomoni.

Baada ya bosi huyo kumfumania ghafla na kuipakia video hiyo kwenye mtandao wa Twitter, klipu hiyo imesambazwa sana huku watu wengi wakitolea shuhuda zao jinsi walivyowafumania wafanyikazi wao wa ndani wakifanya matukio ya kushangaza.

“Siwezi kuamini mtu wa kazi za kukarabati kwangu kweli alikuwa amekaa kwenye kochi langu akinywa divai yangu kutoka kwa chupa,” bosi huyo mwanamke kwa jina @iAdoreNelly alifunguka huku akipakia video hiyo ya huyo jamaa mnene akiiba divai. Kutoka kwa chupa.

“Kwa upande wangu, ninachofanya ni kuwatazama kwa makini watu wanaokuja kufanya usafi katika nyumba yangu. Sitaki kamwe kuwa mwathirika,” mmoja aliandika.

Mwingine alielezea jinsi kijakazi alijitoma ndani ya chumba chake bila hodi wakati anavaa nguo na kusema tangu tukio hilo aliapa kutoishi na mfanyikazi tena.

“Hii ndiyo sababu sitawahi kuishi mahali fulani na house boy ambaye anaweza kuingia mahali pangu tena. Baada ya kumpata anaingie chumbani kwangu bila kutangaza nikiwa nabadilisha  nguo chuoni na hakuondoka nilipompigia kelele atoke kihalisi kamwe. Nilichukia kwamba alikuwa na funguo za mlango,” mwingine alielezea.

Mwingine ambaye alionekana kuwa bosi alieleza siku aliporudi nyumbani mapema kutoka kazini na kumpata msichana wa kazi za ndani akiwa amejibwaga kwenye kiti chake huku akinywa divai na kusoma gazeti lake na miguu ameitupa mezani raha tupu.

“Nakumbuka nilirudi nyumbani mapema kuliko kawaida na kumkuta yule mwanamke wa kusafisha akiwa ameketi kwenye kochi langu akiwa ameshika glasi ya divai nyekundu, akipitia gazeti langu la Vogue, huku miguu yake ikiwa juu ya meza ya kahawa akiwa amevalia viatu vyangu,” mtumizi wa Twitter kwa jina Ann Thomas alieleza.