Mjasiriamali Hamisa Mobetto ameshangazwa kwamba hawezi kabisa kuamini siku hizi watu wanamuona bure bilashi bila hata kulipia senti moja.
Mobetto anasema kwamba wale wanaomuona bure wana bahati sana na jambo hilo haamini kabisa katika maisha yake.
"Siwezi kuamini watu wananitazama bure, wana bahati sana!" hamisa Mobetto alidokeza kwenye picha yake maridadi Instagram.
Mwanamama huyo amabye ni mzazi mwenza wa msanii namba moja wa muda wote ukanda wa Afrika Mashariki Diamond Platnumz alidokeza kwamba yeye katika hali ya kawaida watu wanafaa kumtazama pindi tu wanapolipia huduma hiyo.
Licha ya na urembo wa kudumu, wengi walikuwa wanadhani mama huyo wa mtoto mmoja alikuwa anasaidiwa kimaisha na mzazi mwenzake Diamond Platnumz, jambo ambalo katika siku za hivi karibuni amekuwa akilikanusha na hata kuweka wazi kwamba hawashirikiana kulea mtoto na Diamond bali ni kujitutumua binafsi tu kwa ajili ya maslahi ya mtoto.
Mwezi jana aliweka wazi kwamba Diamond aligoma kitambo kumsaidia katika malezi ya mtoto na hata kusema hajui ni kwa nini msanii huyo hakumtakia heri njema ya kuzaliwa mwanao kama ilivyokuwa miaka ya awali.
Pia jana baada ya msanii Baba Levo kumtania kwamba naye asije kusema Diamond hamsaidii kwani watu wa karibu naye wanajua anamwaga pesa kwa ajili ya mtoto, Mobetto alimjia juu chawa huyo wa WCB kwa kusema kwamab yeye hajawahi mwagiwa pesa na kama kweli anajua pahali zinamwagwa basi wakaondoke pamoja kuziokota.