Rais Ruto Mlinde Mama wa taifa dhidi ya Wachungaji hawa - Andrew Kibe

Watu wamekuwa na mgawanyiko mitandaoni kuhusu uchamungu wa rai Ruto na mama wa taifa Rachael Ruto.

Muhtasari

• Mwambie mkewe kuzingatia katika kukuhudumia na wewe kuzingatia katika kuendesha nchi - Kibe

Kibe amtaka Ruto kumlinda mkewe dhidi ya wachungaji
Kibe amtaka Ruto kumlinda mkewe dhidi ya wachungaji
Image: Facebook

Siku chache baada ya kuapishwa kwa Ruto kama rasi wa tano, kumekuwa naminong’ono mingi mitandani kuhusu jinsi rais huyo na mkewe wanavyojiweka kwa njia ya Kikristu.

Jana msanii mkongwe wa injili na aliyekuwa mgombea urais kabla ya IEBC kumfungia nje, Reuben Kigame alizua mjadala Twitter akidai kwamba serikali ya Ruto inatumia Biblia na ucha Mungu vibaya.

Wengi waliachwa vinywa wazi na matamshi haya kutoka kwa mwinjilisti huyo, hay ani baada ya mama taifa Rachael Ruto kuwakaribisha watumishi wa Mungu mbalimbali katika ikulu ya Nairobi.

Watu wamekuwa wakigawanyika kuhusu mjadala huo huku wengine wakisema Ruto na mama taifa hawafai kukaribisha machungaji na wahubiri katika ikulu huku wengine wakisema ni sawa kwani ndio hatua nzuri ya kuonesha nchi kuwa ya wachamungu kutoka kwa kiongozi wa taifa.

Mwanablogu Andrew Kibe naye hajaachwa nyuma katika kulitilia suala hilo kweney mizani. Kupitia YouTube yake, Kibe alimtaka rais William Ruto kumlinda mkewe kutoka kwa wachungaji hawa wote wanaotaka kukutana naye kweney ikulu kwani wengine ni jina na umaarufu tu wanataka kujizolea kupitia jina la mama Rachael na ikulu kwa ujumla.

“Rais mchunge mkewe kutokana na wachungaji hao wanafiki. Hao wachungaji watatuharibu si watu wazuri. Baadhi yao ni watu wabaya sana, mwambie mkewe kuzingatia katika kukuhudumia na wewe kuzingatia katika kuendesha nchi, hayo mengine ni ya uongo,” Andrew Kibe alisema.

Kulingana na Kibe, aliwataka viongozi kuwaweka wake zao mbali na uongozi haswa wa taifa na wakome kuwaweka kwenye mwanga wa kushughulika na masuala ya uongozi kwa kile alisema wananchi walimchagua yeye na si mkewe.

Juzi mama Rachael kupitia kwenye Twitter yake alidokeza kwamba aliwapokea na kuwakaribisha wachungaji katika ikulu ya Nairobi, siku chache tu baada ya kuhamia ikuluni.