"Sijawahi kuhisi hivi maishani!" Akothee ajigamba kuhusu mahusiano yake mapya

Akothee amejivunia kuwa sasa amepata mzungu mdogo , tofauti na wazungu wazee aliowahi kuwa nao hapo awali.

Muhtasari

• Akothee amekiri kuwa hajawahi kuhisi vizuri jinsi anavyohisi sasa  akiwa kwenye mahusiano yake mapya.

•Alisema kwa sasa anachumbiana na mwanaume huyo pekee na kubainisha kuwa hayupo kwenye mahusiano mengine ya kando.

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Kwa kweli mwimbaji na mjasiriamali mashuhuri Esther Akoth almaarufu Akothee amezama kabisa kwenye dimbwi la mahaba.

Mama huyo wa watoto watano amejitosa kwenye mahusiano na mwanaume mzungu ambaye ni maelezo machache tu yanayojulikana kumhusu.

Katika chapisho lake la hivi punde, Akothee amekiri kuwa hajawahi kuhisi vizuri jinsi anavyohisi sasa  akiwa kwenye mahusiano yake mapya.

"Tuko Alba Italia, sijawahi kuhisi hivi katika miaka yangu yote 40, Mniruhusu nijifurahishe," Akothee aliandika kwenye Instagram chini ya picha yake na mpenziwe  iliyopigwa  wakati wa ziara yake Italia mnamo Agosti 8.

Pichani, yeye na mpenziwe mwenye umri wa makamo walionekana wakiwa wamekumbatiana na kufurahia muda pamoja.

Alisema kwa sasa anachumbiana na mwanaume huyo pekee na kubainisha kuwa hayupo kwenye mahusiano mengine ya kando. Pia alionekana kujivunia kuwa sasa amepata mzungu mdogo , tofauti na wazungu wazee aliowahi kuwa nao hapo awali.

"Wee kama angekua guka ,zile matusi ningepokea , ni Mungu tuu. Mungu wa Akothee akupate pia .Nakupenda mpenzi❤," alisema katika chapisho lingine.

Aliongeza, "Ninachumbiana na mwanaume mmoja kwa wakati mmoja, nina moyo mmoja tu, nikifa nakufa. Niko bize kupenda huyu hakuna wakati kwa mtu mwingine yeyote. Hiyo ndiyo tofauti kati yangu na wewe."