Siku ya Jumatano, Septemba 21, mamake mwanamuziki Nadia Mukami alikuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa.
Nadia alizamia kwenye Instagram kumsherehekea mzazi huyo wake kwa hatua mpya ya maisha aliyopiga.
"Ni siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mama yangu. Heri ya siku ya kuzaliwa Mama Mukami," aliandika.
Malkia huyo wa muziki wa Kenya alimsherehekea mamake kwa utumishi wake mkubwa katika Jeshi la Kenya.
"Ameitumikia nchi hii kwa moyo na roho yake!! Mwanamke jasiri kama huyu," alisema Nadia.
Hata hivyo hakufichua miaka ambayo mzazi huyo wake ametimiza mwaka huu.
Takriban miaka miwili iliyopita mwimbaji huyo aliwanunulia wazazi wake gari ndogo ya kutumia katika safari zao za hapa na pale.
Alitangaza habari hizo kwenye Instagram ambako alichapisha picha za wazazi wake wakiwa wamesimama kando ya gari lao mpya na logbook mkononi.
"Wamiliki wa hivi punde wa gari, Baba na Mama Nadia Mukami, wazazi wangu. Mungu ni mwema wanashikilia logbook yao,” aliandika.
Nadia ana wimbo maalum kwa mama yake 'Saluti kwa mama' ambao aliimba pamoja na Iyanii mwezi Mei mwaka huu.
Katika wimbo huo, Nadia anamshukuru mzazi huyo wake kwa jitihada zote ambazo aliweka kumlea.
Saluti kwa mama
Heshima kwa mama
Pongezi mama
aSaluti kwa mama
Mapenzi kwa mama
Asante mama Saluti kwa mama
Heshima kwa mama
Pongezi mama
Saluti kwa mama
Mapenzi kwa mama
Asante mama
Ulijinyima ndio nipate
Zile Mateso nisikose
Ulinipa vyako vyote," Maneno ya wimbo huo yanasema.
Katika wimbo huo Nadia anamuombea mama yake maisha marefu hapa duniani.