Kijana mmoja alizua tafrani kwenye mitandao ya kijamii baada ya kudai kwamba ana pesa nyingi ambazo alikuwa amejiratibu muda wa miaka miwili ili kumalizka kuzitumika.
Kijana huyo aliyetambulika kwa jina Kwame Amerika kutoka Ghana alifichua kwamba amebakiza miaka miwili kutumia bilioni 2 za Ghana ambazo ni sawa na milioni 24 pesa za Kenya.
Hii ni baada ya Kupakia video ambayo inamuonesha akishiriki katika matukio mbali mbali katika mchakato wa kumaliza pesa hizo kwa nyakati tofauti. Mwanamume huyo aliwaomba wanamtandao kumweka katika maombi ili aweze kutimiza lengo lake la kuhakikisha bilioni mbili sawa na bilioni 24 za Kenya hizo zinakamilika katika muda aliopewa.
Mwanaume huyo mdogo alitambulika kwa jina Kwame Amerika alisema kwamba pesa hizo anafaa kuzitumia kwa kitu chochote cha kumpa furaha maishani mwake ikiwemo kutembelea familia za watoto mayatima, kuwasaidia maskini na wakimbizi miongoni mwa mambo mengine ambayo ni kusaidia jamii na kuupa moyo wake furaha ya kudumu.
Katika video hiyo kwenye TikTok, Kwame Amerika anaonekana akiwapa watu pesa akiwa juu yagari la kifahari na sehemu nyingine kwenye video hiyo hiyo anaonekana akitoa msaada wa chakula wa familia moja, yote tu kama njia moja ya kujifurahisha kwa kutumiabilioni mbili yake.
Aliwataka watu kumtajia njia zingine ambazo ataweza kuzitumia pesa hizo kabla ya muda kukamilika na kuwataka wengine wenye hitaji la msaada kuweka namba zao ili pia awakwamue.
“Niombeeni rafiki zangu nina miaka miwili iliyosalia kumaliza kutumia bilioni 2 zangu. Lengo ni kumfanya kila mtu kuwa na furaha, kuwasaidia wasiojiweza na maskini pia. Toa maoni yangu ukisema ni kiasi kipi haswa cha pesa unahitaji,” kijana huyo aliandika kwenye video ile.
Watu walishindwa kujizuia haswa baada ya kipande cha mwisho cha video hiyo kumuonesha kaketi kama vile anafanya tambiko au ramli.