Mimi sio mkurugenzi wa Mawasiliano katika ofisi ya DP Rigathi Gachagua-Jacque Maribe

Hii ni baada ya ujumbe ulioshirikiwa na rafiki yake ukisema kwamba yeye ni mkurugenzi wa mawasiliano.

Muhtasari
  • Hii ni baada ya kupokea simu na jumbe nyingi za pongezi kutoka kwa marafiki na mashabiki wake
  • Maribe kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alikanusha madai hayo, huku akisema hayo ni mambo ya Mungu
Jacque Maribe
Jacque Maribe
Image: hisani

Hatimaye Aliyekuwa mwanahabari wa runinga ya Citizen Jacque Maribe, amejitokeza wazi wazi na kuzungumzia madai kwamba ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa mawasiliano katika ofisi ya naibu rais.

Hii ni baada ya kupokea simu na jumbe nyingi za pongezi kutoka kwa marafiki na mashabiki wake.

Maribe kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alikanusha madai hayo, huku akisema hayo ni mambo ya Mungu.

Hii ni baada ya ujumbe ulioshirikiwa na rafiki yake ukisema kwamba yeye ni mkurugenzi wa mawasiliano.

Ujumbe huo ulisoma;

“Mkurugenzi wa Mawasiliano mtarajiwa katika ofisi ya Naibu Rais Rigathi Gachagua Jacque Maribe amejikusanya kiujasiri,” alisema Nzau.

Katika chapisho hilo, Nzau aliendelea na kusema Maribe ambaye awali alitupilia mbali ahadi ya kufunga pingu za maisha na Katibu mtarajiwa wa baraza la mawaziri la Kenya Kwanza, Dennis Itumbi, sasa huenda tena mwanablogu huyo amekuja na ombi jipya kwake.

Huku Maribe akijibu madai hayo alisema kuwa;

"Mimi sio mkurugenzi wa mawasiliano katika ofisi ya naibu rais Rigathi Gachagua,asanteni kwa jumbe zennu za pongezi, mambo ya Mungu," Aliandika Maribe.