P-Square wafunguka sababu za kutengana kwa miaka 6

Wawili hawa wamerudi na majina ya majazi mapya, Paul akitambulika kama Rudeboy na Peter akitambulika kama Mr. P.

Muhtasari

• Wameanza ziara katika miji 100 duniani kote, Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Tanzania, na London kati ya nchi nyingine.

Peter Okoye, Paul Okoye
Image: P-Square (Instagram)

Pacha wa kikundi cha muziki P-Square, Paul Okoye amezungumza baada ya kutengana na kakake Peter Okoye na kupotea kwenye sekta ya muziki kwa miaka sita.

Paul  alitoa sababu za kutengana kwao , na kwa mara ya kwanza tangu wawili hao kurudi pamoja na kulipa kundi la P-Square uhai tena, mashabiki wameweza kujua kiini cha uadui wao awli.

Baada ya kurudiana tena, wawili hao ambao ni mapacha walitimba kwenye studio na kurekodi kibao kimoja cha moto - Jaiye - dude amablo limepata mapokezi ya aina yake kutoka kwa mashabiki waliokuwa wamewakosa sana wanamuziki hao wa damu moja.

Alipoulizwa chanzo cha kutengana kwao, Paul alisema kuwa Shetani alikuja kati yake na pacha mwenza na kuweka wazi kuwa hawapangi kutengana tena.

Hapo awali Paul alikuwa amefichua chanzo cha kutengana kwao kilikuwa mambo ya kifamilia na si ya kimuziki.

“P-Square ilikuwa dhabihu, sikusema chochote kwa sababu nlijua chanzo kilikuwa gani,” alisema.

Aliongeza kuwa suala hilo la familia lililotokea lilifanya muungano wake na kakake wa kundi lao la P-Square kulipia na mwishowe kusambaratika.

Hata hivyo, Paul hakuongelea suala hilo wala kusema ni shida gani haswa ya kifamilia ilisababisha kutengana kwao.

“Haikua na mahusiano yoyote na muziki, na kwa sababu ya upendo kwa familia yangu , sitaeleza chochote,” alisema.

Baada ya kutengana kwao wawili hawa wamerudi na majina ya majazi mapya, Paul akitambulika kama Rudeboy na Peter akitambulika kama Mr. P.

Wawili hao wamekuwa kwenye ziara yao ya muziki ya miji ya dunia.

Katika video ya instagram kwa akaonti ya Rudeboy, waimbaji ya kibao cha 'Do Me' walitangaza kuwa wanaanza ziara katika miji 100 duniani kote, Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Tanzania, na London kati ya nchi nyingine

''Unajua nini,ni wakati wa  Psquare na tutazuru miji 100 duniani kote,Kenya, Tanzania Afrika Mashariki kote, London, United States. Zitaje,nyimbo mbili mpya zinakuja '' Psquare walisema.

Wanamuziki hawa waliweza kutoa nyimbo zilizotamba sana kabla ya kutengana kwao zikiwemo: No One Like You, Collabo, Kidogo (waliyofanya na mwanamuziki Diamond) zikiwa miongoni mwa zingine.