logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+videos) Mlinzi wa lango agongesha gari la bosi wake baada ya kuliendesha bila idhini

“Kwa taarifa yako kijana alitumia gari la mama mwajiri wake kujifunza kurudisha nyuma wakati mama hakuwa karibu - Tony aliandika.

image
na Radio Jambo

Habari26 September 2022 - 07:00

Muhtasari


• Mama yangu alimpa ufunguo wa gari ili aupatiane kwa mtu mwingine kwa sababu nilikuwa nimelala - kijana wa mwajiri alisema.

Kijana mmoja ambaye ameandika katika boma kama mlinzi wa lango alijipata pabaya baada ya kujarfibu kuliendesha gari la mwajiri wake na kuligongesha akijaribu kurudisha nyuma.

Katika video iliyozua gumzo pevu kwenye mtandao wa TikTok, mwenye kuipakia alisema kwamba kijanaq huyo alikuwa anataka kutamba kwa wenzake kuwa anajua kuendesha na kuishia kwa kuligongesha gari kweli ukuta wa lango.

Mwenye kupakia video hiyo ni mtoto wa mama mwajiri wa kijana huyo mlinzi wa lango na kwenye klipu hiyo ambayo anasikika akizungumza kwa kejeli na vicheko vya kebehi, aliandika kwamba mlinzi wa lango lao alikuwa anatumia gari la mama yake kujifunza pasi na idhini kutoka kwa mama.

“Jamaa huyu aligongesha gari kwenye lango. Mama yangu alimpa ufunguo wa gari ili aupatiane kwa mtu mwingine kwa sababu nilikuwa nimelala, badala yake yeye akaingia ndani ya gari na kuanza kuliendesha,” mtoto wa tajiri alimjibu mtu mmoja aliyetaka kujua tukio zima lilianza vipi.

Wengi walitaka kujua tukio zima haswa baada ya kijana huyo kuandika maandishi ya kutatiza kichwa kwenye video hiyo kwamba, “Kwa taarifa yako kijana alitumia gari la mama mwajiri wake kujifunza kurudisha nyuma wakati mama hakuwa karibu,”

Wengine walisema kwamba alifanya kitendo cha kuotesha kibarua chake nyasi na kumtaka atoroke kabla mama mwajiri wake hajagundua.

“Mimi ningekuwa yeye, ningekuwa nimechana mbuga kabla mama ajue,” mmoja kwa jina That Girl aliandika.

“Kijana nafikiri atakuwa ametoroka ifikapo asubuhi mapema,” Toni Akerele ambaye ni mtoto wa mama mwajiri na mwenye video ile alijibu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved