Wikendi iliyopita baada ya tukio la kushambuliwa kwa kitu kilichodhaniwa kuwa aside kwa msanii wa Mugithi Joyce Wamamaa katika klabu moja alikokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, sasa wale waliotuhumiwa kusababisha kitendo hicho wamejitoa kujitetea.
Mwimbaji wa nyimbo za Kikuyu Wanja Asali ambaye alituhumiwa kuwa ndiye aliyemmwagia Wamamaa kemikali ilwe amejitenga mbali na madai hayo kwa kusema kuwa hakuhusika kwa njia yoyote kumdhuru Wamamaa.
Inaarifiwa Wamamaa alilazwa hospitalini baada ya kitu kiowevu kumwagwa kwenye uso wake, kile amabcho wale waliohudhuria kwenye sherehe hiyo walimnukuu akisema alikuwa anawashwa macho na ngozi ya mwili.
Polisi katika eneo la Kayole wanaendela na uchuguza wa kiini cha tukio hilo ambalo lilitajwa kuwa shambulio ambalo karibia limpofue msanii huyo wa kibao moto – Wendo Wi Cama.
Ripoti zinaonyesha kuwa mwanamuziki huyo kwa sasa amelazwa hospitalini huku juhudi za kurejesha uwezo wake wa kuona zikiendelea.
Hata hivyo, Joyce wa mamaa anasema yuko mzima baada tukio hilo.