Kunani? Bahati afuta machapisho ya Instagram baada ya Diana kupakia ujumbe wa wasiwasi

Diana Marua pia amedokeza kuwa kuna kitu kisicho sawa nyumbani kwao.

Muhtasari

•Siku za hivi majuzi wanandoa hao wamesalia kimya na hata kuepuka vyombo vya habari, jambo lisilo kawaida yao.

•Bahati sasa amezifuta picha na video zote zilizokuwa kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Image: INSTAGRAM// BAHATI

Huenda kuna kitu ambacho sio sawa nyumbani kwa mwimbaji wa nyimbo za mapenzi Kelvin Kioko almaarufu Bahati.

Baada ya kusalia kimya kwa muda mrefu tangu azma yake ya kuwania ubunge wa Mathare kukosa kufua dafu, mwanamuziki huyo sasa amezifuta picha na video zote zilizokuwa kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kabla ya kuchukua hatua hiyo ya kushangaza, kurasa za Bahati za mitandao ya kijamii ambazo hapo awali kabla ya uchaguzi zilikuwa na shughuli nyingi hazikuwa na chapisho lolote mpya tangu Agosti 12.

Chapisho lake ka  mwisho lilikuwa, "Siku 3 baada ya uchaguzi kufanyika, masanduku 21 yameharibiwa. Nimekuwa nikisubiri kutangazwa mshindiu na kupewa cheti rasmi kama mbunge mteule wa Mathare," 

Bahati ambaye aliwania kwa tiketi ya Jubilee aliibuka wa tatu katika kinyang'anyiro cha Agosti 9, nyuma ya Anthony Oluoch wa ODM na Billian Ojiwa wa UDA. Alijizolea kura 8,166 huku Olouch akinyakua kiti kwa kura 28,098. Ojiwa alipata kura 16,912.

Mkewe Bahati na ambaye mama ya watoto wake wawili, Diana Marua pia amedokeza kuwa kuna kitu kisicho sawa nyumbani kwao.

Chapisho la mwisho la mtumbuizaji huyo liliwaacha mashabiki wake na wasiwasi mwingi wasijue kinachoendelea katika maisha yake. Alipakia picha ya njiwa aliyebeba jani na kuandika, "Katika giza tu, unaweza kuona nyota"

Siku za hivi majuzi wanandoa hao wamesalia kimya na hata kuepuka vyombo vya habari, jambo lisilo kawaida yao. Wawili hao hata hawajakuwa wakitoa taarifa kuhusu maendeleo ya ujauzito wao kama ilivyokuwa awali.

Mapema mwezi huu Diana Marua alidokeza kuwa siku yake ya kujifungua mtoto wa tatu ilikuwa imekaribia.

"Huu umekuwa ujauzito wangu mfupi zaidi kuwahi kutokea. Siamini kuwa karibu naelekea hospitalini kupokea bando langu la furaha. Tarehe ya kujifungua imepangwa !!!," Diana Marua alisema.

Mama huyo wa watoto wawili alieleza hamu yake kubwa ya kukutana na mwanawe. Hata hivyo alidokeza kuwa hayuko tayari kwa mchakato wa kujifungua.

"Lakini kusema kweli mimi siko tayari kwa thieta, ni jinsi ninavyotazamia kukutana na mtoto inanipa nguvu. Hebu tufanye hivi," alisema.

Diana na Bahati walitangaza ujauzito wa mtoto wao wa tatu pamoja mwezi Julai kupitia wimbo "Nakumbolov."