Jimal amjibu mtu aliyesema anajipendekeza kwa wanasiasa,"wewe kwa landlord!"

Jimal amekuwa akijibizana na mashabiki wake wengi katika siku za hivi karibuni.

Muhtasari

• “Wewe unapenda kujipendekeza kwa mwenye nyumba,” Jimal alijibu

Jimal Rohosafi akiwa na spika wa bunge la kitaifa
Jimal Rohosafi akiwa na spika wa bunge la kitaifa
Image: Instagram

Mfanyibiashara maarufu katika sekta ya matatu Jimal Rohosafi kwa mara nyingine amejipata katika mzozo mkali na watumizi wa mtandao wa Instagram.

Jimal alipakia picha wakiwa na spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula na kusema kwamba ilikuwa ni Jumapili laini yenye utulivu ambapo alikuwa anapunga upepo na kiongozi huyo wa bunge.

Mashabiki na watumizi mbali mbali walimjia juu huku wengine wakimsuta kwamba wanamwelewa kupunga upepo na kila mtu kwa sababu ni mpweke, haswa kufuatia kusambaratika kwa mahusiano yake na aliyekuwa mkewe, Amira.

Mwingine pia alimkandia kavu kwa kumwambia kwamba ana mazoea ya kujipendekeza kwa kila mtu ili kupata tu kuzungumziwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Unapenda kujipendekeza kwa wanasiasa,” mtumizi wa Instagram kwa jina Bentah Johns alimwambia bila woga.

Kati ya maombi mbali mbali yenye masimango makali, hili lilionekana kuwa kisu kikali kilichogusa mfupa wa muundi wa guu la Jimal ambaye alishindwa kujizuia na kujibu mipigo. Alimwambia mwanadada huyo kwamba ni heri yeye anapenda kujipendekeza kwa wanasiasa ila huyo yeye anajipendekeza kwa mwenye nyumba ya kupanga.

“Wewe unapenda kujipendekeza kwa mwenye nyumba,” Jimal alijibu huku watu wakicheka kwa jibu hilo.