Unaambiwa katika dunia hii, kitu kikubwa sana na ambacho unaweza ukakifanya katika maisha ya mtu ni kuwasha taa za tabasamu katika nyuso za wale wanaohitaji msaada, haswa watoto wachanga ambao hawawezi kujifanyia vitu vingi tu.
Kuna video moja ambayo imewagusa wengi kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonyesha mama mmoja ambaye hana mikono akitumia mdomo wake kumlisha mwanawe mchanga kabisa.
Katika video ya mtandaoni iliyoonekana kwenye TikTok, mama huyo alionekana akichukua chakula vizuri na kumpa mtoto, jambo ambalo limewafurahisha sana wanamitandao kwa jinsi mama huyo alikuwa anaweka umakini na weledi mkubwa kuhakikisha mtoto wake anapata kushtaki njaa.
Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la @miminefanmvanyan2 ni mlemavu kwa kuwa inaonekana ni mlemavu wa viungo. Lakini mapungufu yake hayakumzuia kamwe kutomlisha mwanawe. Alitumia mdomo kama mbadala ya vidole vya mkono na kushikilia kijiko ambacho alikuwa anachotea chakula na kukielekeza mdomoni mwa mwanawe aliyekuwa akikipokea kwa furaha tele.
Video hii iliwafurahisha wengi ambao walisema kweli mama hata awe kilema atabaki kuwa mama tu na hakuna chapa nyingine ya mama isipokuwa yule tu aliyekuzaa.
“Ni baraka iliyoje mama. Ndio maana nachukia kuona wanaume wanamtendea vibaya malkia kwa sababu wao ni warembo na wana nguvu za ajabu,” Anna Sterling aliandika.
Mwingine kwa jina April Green naye aliandika, “Mama daima anajua jinsi ya kutunza watoto. Upendo wa mama. Asante kwa akina mama wote.”
"Ninajivunia kuona mama anayefanya kazi kwa bidii kama wewe! upendo mkubwa kwa akina mama wote duniani" mwingine aliandika kwa furaha.