Mwisho wa siku nitarudi kwako tu! - Rapudo adokeza kurudiana na Amber Ray

Wewe ni kitu kizuri ambacho kiliwahi nitokea maishani mwangu - Rapudo.

Muhtasari

• Mwisho wa siku nitarudi kwako nikikimbia, si kwa sababu mimi ni mnyonge bali ni kwa sababu nilizama katika bahari ya mapenzi na wewe - Rapudo.

Amber Ray na Rapudo kwenye Mtoko huko Lamu
Image: RAPUDO//INSTAGRAM

Mwanafasheni Amber Ray na Kennedy Rapudo wamedokeza kurudiana baada ya kuachana kwa mwezi mmoja.

Rapudo alichapisha picha kwenye mtandao wake wa Instagram  iliyoandikwa:

'Mwisho wa siku nitarudi kwako nikikimbia, si kwa sababu mimi ni mnyonge bali ni kwa sababu nilizama katika bahari ya mapenzi na wewe, siwezi kuwa bandia kuigiza kuwa mgumu, hiyo ni ya watu wapweke," Rapudo aliandika kwenye Insta story yake.

Vilevile, Rapudo alizidi kueleza matukio yaliyomtokea baada ya Amer Ray kumbwaga mwezi mmoja uliopita. Alieleza kuwa kwa wakati mmoja alijaribu kuwa nunda ila maji yakazidi unga mambo yalipomkaba hadi kwenye koo mpaka kushindwa kufanya mishe za kila siku. Aliongeza kuwa Ray ndiye kitu bora zaidi kichowahi tokea katika maisha yake.

"Nilijaribu kujifanya mgumu lakini naweza sema ukweli wakati ulipoondoka ulienda na kila kitu kizuri kilichokuwa ndani yangu, kitu kizuri ambacho kiliwahi nitokea maishani mwangu," Rapudo alitema nyongo.

Amber Ray na Rapudo wameonekana pamoja huko Lamu wakila bata na kuzichapisha picha zao maridhawa kwenye kurasa za Instagram.

"Mara ya kwanza kuja Lamu na nimekupenda sana,"alisema mwanafasheni huyo huku Rapudo akichapisha Instagram video na picha wakiwa pamoja.

Amber Ray alisema kuwa Rapudo akiendelea kumzawadi kwa kumpa maua atambebea uja uzito na kumzalia.

"Anapofananisha maua anayokupa na nguo ulizovaa. Siri nichezee wimbo wa 1000 stems na yeye," mwanafasheni alisema huyo aliyekuwa na furaha tele.

Amber Ray hakusema alipokea maua hayo kutoka kwa nani haswa, jambo lililowaacha mashabiki wake wakikisia aliyekuwa amemzawadi mwanadada huyo.

Mashabiki wengine waliweza kujaza haba na haba kupata kibaba na kufichua kuwa Amber Ray alikuwa kwenye gari la Rapudo huku wengine wakidhani maua hayo yametoka kwa Jimal.

Mashabiki wa Rapudo waliwaonyesha Amber Ray na Rapudo upendo na kushangilia kurudiana kwao.